Tuesday, September 18, 2012

VODACOM YAZINDUA OFA YAKE MPYA YA BONGA


* Wasteja kupiga simu kwa mtandao wanje kwa Tsh1.5, asilimia 50 kutoka kwa Tsh3.
* Ili kujiunga kutumia huduma hiyo wateja wanatakiwa kubonyeza  *149*01#.

DAR ES SALAAM, TANZANIA
Dar es Salaam, Septemba 18, 2012 ... Wateja wa simu za mikononi wanayo sababu za kuendelea kupiga simu kufuatia  kuzinduliwa kwa ofa mpya itakayo wezesha wateja kupiga simu kwa asilimia 50 nafuu

Kampuni ya simu ya Vodacom imezindua ofa inayoitwa Bonga tariff itakayo wezesha wateja kupiga simu kwa mitandao yote kwa Tsh 1.5 kwa sekunde
Kwa mujibu wa Meneja Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Rene Meza, wateja wanafaa kupiga *149*01# ili kujiunga na ofa hiyo

“Hakuna makato yeyote ya takayokatwa katika huduma hii mpya, ila kwa mtu ambaye ataamua kutoitumia atalipishwa Tsh100,” alisema Meza.
Wateja wa Vodacom pia wataendelea kutumia ofa zingine kama vile cheka bundles wakati huduma hii ikiendelea.
Meza alieleza kuwa kampuni ya Vodacom itaendelea kuwapa wateja wake huduma zinazo faa na kuongeza kuwa ili kuboresha Biashara wateja wanafaa kuridhika na huduma wanazopewa.

“Tunaishi katika Dunia ambayo inaitaji kila mtu awasiliane na wenzake na pia wapendwa wake kwahivyo ni muhimu kuwawezesha kuwasiliana kwa bei nafuu,” alisema Meza na kuongezea, “Tunawashukuru wateja wetu kwa ushurikiano wao na tunawaomba wanufaike na ofa hii.”

0 comments:

Post a Comment