Meneja mahusiano wa TBL Doris Malulu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya uzinduzi wa kampeni kubwa ya vinywaji hivyo kuwatembelea watumiaji majumbani mwao na kutoa elimu juu ya umuhimu wa kutumia vinywaji vilivyo bora , Kampeni hiyo itajulikana kwa jina la Nyumbani ni Nyumbani na itajumuisha mikoa kumi ya Tanzania Bara,Kulia ni meneja wa vinywaji hivyo Consolata Adam.
Na Mwandishi Wetu
KATIKA kile kinachoonekana kusogeza huduma bora zaidi kwa wananchi na kutambua umuhimu wa afya zao, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia vinywaji vya Grand Malt na Vita Malt imezindua kampeni maalumu iitwayo ‘Nyumbani Ni Nyumbani’ kwa ajili ya kupeleka bidhaa hizo zisizo na kilevi kwa Watanzania wote.
Akizindua kampeni jijini Dar es Salaam jana, Meneja Bidhaa zisizo na vileo wa TBL, Consolata Adam alisema, wamezindua kampeni hiyo maalumu ili kuhakikisha vinywaji visivyo na kilevi vinamfikia kila mtu.
“Tumeamua kuzindua kampeni hii ili kuhakikisha kila Mtanzania anafahamu umuhimu wa vinywaji vya Grandmalt na Vitamalt katika matumizi ya kutunza na kulinda afya zao.
“Kampeni hii itahusisha mabalozi wa Grand Malt na Vita Malt kwa pamoja kutembea nyumba kwa nyumba na kuhakikisha ujumbe huu unamfikia kila mtu katika nyumba yake ambapo pia kutakuwa na fursa ya kujishindia na kuzawadiwa zawadi mbalimbali wakati wa kampeni hiyo,” alisema.
Consolata alisema, vinywaji hivyo ni vizuri zaidi kwa afya ya mwanadamu kwani vimet engenezwa vikiwa na virutubisho vya kila aina na vinafaa mno hata kwa mama mjamzito.
“Tunaomba Watanzania wasishangae pale watakapokutana na watu wetu ambao watakuwa wanawatembelea majumbani kwao, kwani lengo ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata fursa ya kutambua faida za kutumia kinywaji cha Grand Malt na Vita Malt katika kulinda afya yake ili tuweze kujenga desturi ya kuwa na matumizi bora kwa ajili ya kujenga afya zetu,” alisema.
Nayee Afisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu alisema hii ni kampeni ya kwanza kuzinduliwa na vinywaji hivyo kwa lengo moja la kuwawezesha Watanzania kutumia bidhaa hizo zenye faida kubwa kwa mwili wa mwanadamu.
“Tunataka bvinywaji hivi vipatikane kila mahali na pia kuwasaidia Watanzania umuhimu wa kuvitumia kwani vina faida kubwa kwa wote, kuanzia hata kwa mtoto,” alisema Doris.
Kampeni hiyo ya ‘Nyumbanio ni Nyumbani’ inatarajiwa kuanza katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Mtwara, Dodoma, Iringa, Morogoro, Mbeya na Shinyanga ambapo itaanzia mji wa Kahama.
Vinywaji vya Grand Malt na Vita Malt ambavyo havina kilevi vinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
0 comments:
Post a Comment