This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Monday, December 23, 2013

GHARAMA ZA UMEME ZAPANDA TENA


Mkurugenzi wa Usimamizi wa Uchumi wa amlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi akitangaza bei mpya ya umeme jana katika mkutano na waandishi wa Habari Dar es Salaam. Kulia kwake  ni Mkurugenzi wa Umeme wa mamlaka hiyo, Anastas Mbawala. (PICHA  NA RICHARD MWAIKENDA

TAARIFA KAMILI
Tarehe 11 Oktoba 2013, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liliwasilisha maombi ya kurekebisha bei ya umeme kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). TANESCO ilipendekeza kuongeza bei kwa asilimia 67.87 kuanzia tarehe 1 Oktoba 2013, asilimia 12.74 kuanzia tarehe 1 Januari 2014 na asilimia 9.17 kuanzia tarehe 1 Januari 2015. Vilevile TANESCO waliomba kuidhinishwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumuko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya kitanzania. Aidha, TANESCO iliomba kuidhinishwa viwango vya gharama za kuunganisha umeme vinavyozingatia ruzuku inaliyotolewa na Serikali, na kuidhinishwa tozo mbalimbali kwa huduma zitolewazo na TANESCO.

Kwa mujibu wa TANESCO, kupitishwa kwa maombi haya kutaliwezesha Shirika (a) kupata fedha za uendeshaji na uwekezaji wa miundombinu, (b) kulifanya Shirika liweze kukopesheka na hivyo kuwezesha kupata mikopo yenye masharti nafuu, (c) kuliwezesha Shirika kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme kwenye Gridi ya Taifa, na (d) kuongeza uwezo wa kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya miundombinu iliyopo ili kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa huduma za umeme wa uhakika kwa wateja.

Itakumbukwa kwamba bei za umeme zinazotumika hivi sasa ziliidhinishwa mwezi Januari 2012. Bei hizo zilipanda kwa asilimia 40.29 ikilinganishwa na maombi ya TANESCO ambapo ilipendekeza bei zipande kwa wastani wa asilimia 155. Sababu ilikuwa ni kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kulikosababishwa na hali ya ukame katika maeneo yanayotiririsha maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme, toka mwaka 2011. Hali hiyo ilipelekea TANESCO kulazimika kununua umeme kwa gharama kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers). Hali ya maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme bado sio nzuri na hivyo TANESCO itaendelea kununua umeme kutoka kwa wazalishaji wa dharura (Emergency Power Producers).

USHIRIKISHWAJI WA WADAU

Kulingana na Kifungu Na. 19(2) (h) cha Sheria ya EWURA, Mamlaka ilifanya Taftishi ili kupata maoni juu ya ombi la kurekebisha bei za umeme. Ukusanyaji wa maoni ulihusisha pia mikutano minne (4) iliyofanyika Iringa na Shinyanga tarehe 15 Novemba 2013, Bagamoyo tarehe 20 Novemba na kuhitimishwa Dar es Salaam tarehe 22 Novemba 2013. Aidha, tarehe 6 Desemba 2013, EWURA iliitisha mkutano wa mwisho wa wadau wakiwemo wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini(MEM), TANESCO, Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO), Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania, Baraza la Watumiaji na Baraza la Ushauri la Serikali, Umoja wa Wazalishaji wa Saruji wa Afrika Mashariki, na kiwanda cha ALAF. Katika mkutano huo EWURA iliwasilisha mwelekeo wa maamuzi kuhusu maombi ya TANESCO na namna zilivyokokotolewa. Wadau walipewa fursa ya kutoa maoni yao kuhusu mwelekeo wa bei na maoni yao yamezingatiwa katika kufikia maamuzi ya mwisho.

UCHAMBUZI NA UAMUZI
Kwa kufuata sheria na kanuni zinazoelekeza kuhusu uchambuzi wa bei ya umeme, EWURA ilifanya uchambuzi wa kifedha na kiufundi ili kubaini uwezo wa TANESCO katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku. Uchambuzi uliangalia utendaji wa Shirika la TANESCO katika miaka iliyopita na pia iliangalia majukumu yanayoikabili TANESCO katika miaka mitatu ijayo. EWURA imebaini kwamba hali ya kifedha ya Shirika la Umeme sio nzuri. Shirika limeendelea kupata hasara, ambayo iliongezeka kutoka shilingi bilioni 47.3 katika mwaka 2010 na kufikia shilingi bilioni 223.4 mwishoni mwa mwaka 2012. Pamoja na mapungufu ya kiufanisi, sababu kubwa ya ongezeko la hasara ni kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wa umeme ambao TANESCO inanunua kutoka kwa wazalishaji binafsi. Hali hii imelifanya shirika kushindwa kulipa madeni yake ya muda mfupi na ya muda mrefu, ambayo yamelibikizwa na kufikia TZS 456.8 bilioni tarehe 22 Novemba 2013, hali ambayo inatishia uendelevu wa huduma ya umeme hapa nchini.

Mamlaka imetumia Kanuni ya Ukokotoaji wa Bei kama ilivyopendekezwa na AF-MERCADOS wakati wa kukokotoa mahitaji ya mapato ya TANESCO. Kanuni hiyo inawezesha kukokotoa bei zinazolandana na gharama halisi kwenye mfumo wa umeme na kuzigawa kwenye makundi ya watumiaji umeme, kadiri kila kundi linavyosababisha gharama kwenye mfumo wa umeme kwa mujibu wa mahitaji ya Sheria ya Umeme ya 2008 Kifungu cha 23(2)(f).

EWURA imejiridhisha kwamba, ufumbuzi wa matatizo ya kifedha ya TANESCO, unahitaji njia/mikakati miwili itekelezwe kwa pamoja:
kuongeza bei ya umeme ili kufikia bei inayokidhi gharama halisi (Cost Reflective Tariff); na
TANESCO kupata mkopo wa gharama nafuu ama ruzuku kutoka Serikalini ili kulipa limbikizo la madeni ya Shirika.
Bodi ya Wakurugenzi wa EWURA, katika kikao chake cha tarehe 10 Desemba 2013 pamoja na mambo mengine, ilitoa maamuzi ya ongezeko la bei za umeme kwa viwango mbalimbali kwa makundi mbalimbali ya wateja, kama ifuatavyo:
Kundi D1: Hili ni kundi la wateja wadogo wa majumbani, hasa vijijini, ambao hutumia wastani usiozidi wa Uniti 75 kwa mwezi. EWURA imeongeza wigo wa mahitaji ya umeme na kufikia uniti 75 kwa mwezi, lengo likiwa ni kuongeza idadi ya wateja wa TANESCO wanaoweza kulipa kidogo kwa matumizi ya umeme kwa kiwango hicho, na pia kuwahamasisha kutumie zaidi umeme. Awali kundi hili lilikuwa linatunia wastani wa matumizi ya uniti 50 kwa mwezi. Bei mpya ni shilingi 100 kwa uniti moja, kutoka shilingi 60 za sasa, sawa na ongezeko la shilingi 40.
Kundi T1: Hili ni kundi la watumiaji wakubwa wa umeme majumbani, biashara ndogondogo, mashine za kukoboa na kusaga nafaka, taa za barabarani, mabango n.k. Bei iliyoidhinishwa ni shilingi 306 kwa uniti moja, ikiwa ni ongezeko la Shilingi 85 ya bei ya sasa. TANESCO ilipendekeza ongezeko la shilingi 131.
Kundi T2: Hili ni kundi la watumiaji umeme wa kawaida ambao hupimwa katika msongo wa volti 400, na ambao matumizi yao ya wastani kwa mwezi ni zaidi ya uniti 7,500 wateja wafanyabiashara kubwa, viwanda vya kati. Bei ya nishati iliyoridhiwa ni shilingi 205 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 73 ya bei ya sasa. TANESCO walipendekeza ongezeko la shilingi 145 ya bei ya sasa.
Kundi T3-MV: Hili ni kundi la wateja wakubwa kama viwanda vikubwa waliounganishwa katika msongo wa kati (Medium Voltage). EWURA imeidhinisha bei ya nishati kwa kiwango cha shilingi 166 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 45 ya bei ya sasa. TANESCO walipendekeza ongezeko la shilingi 148 kwa uniti moja.
Kundi T3-HV: Hili ni kundi la wateja wakubwa waliounganishwa katika msongo wa juu (High Voltage – Voti 66,000 na zaidi) ikiwa ni pamoja na ZECO, Bulyanhulu, na Twiga Cement. Bei iliyoidhinishwa ni shilingi 159 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la shilingi 53 la bei ya sasa. TANESCO waliomba ongezeko la shilingi 80 kwa uniti moja.

Bei ya umeme itakuwa inarekebishwa kila baada ya miezi mitatu kulingana na mabadiliko ya kiwango na bei za mafuta; mfumuko wa bei, mabadiliko ya thamani ya fedha, na upatikanaji wa ruzuku toka Serikalini.

Vilevile, TANESCO inatakiwa kutekeleza miradi ya uwekezaji iliyoainishwa kwa kutumia fedha zitakazokusanywa kutokana na bei zilizoidhinishwa. EWURA inaweza kurekebisha bei ya umeme ya TANESCO kila mwisho wa mwaka 2014 na/au mwaka 2015 endapo TANESCO itashindwa kutekeleza miradi iliyotajwa katika Jedwali husika. Marekebisho hayo yatatokana na makadirio ya gharama za miradi ambayo haikutekelezwa.

Kutokana na matazamio ya kuwa na mabadiliko makubwa katika uzalishaji wa umeme (generation mix) katika mwaka 2015 na kuendelea, kutokana na matarajio ya kuongezeka kwa kwa upatikanaji wa gesi asilia, EWURA itafanya utafiti kubaini gharama halisi (Cost of Service Study) ya huduma ya umeme kwa wakati huo. Hivyo, bei zilizoidhinishwa zitatumika mpaka mwaka 2016, kama utafiti unaotazamiwa kufanywa hautakamilika kabla ya mwisho wa mwaka 2015.

EWURA ililinganisha bei za umeme kwa kila Uniti, katika nchi za Afrika ya Mashariki, na kuona kuwa bado bei za umeme za Tanzania zipo chini ukilinganisha na bei za katika nchi jirani kama inavyoonyeshwa hapa chini, kwa makundi mbalimbali ya watumiaji umeme.

Wednesday, December 18, 2013

TANZANIA DISTILLERIES LIMITED(TDL) YAZINDUA PROMOSHENI YASHINDANO LA KUMSAKA MSHINDI ATAKAE PATA FURSA YA KWENDA KUTEMBELEA SHAMBA KUTENGENEZA KINYWAJI CHA AMARULA NCHINI AFRIKA KUSINI LIJULIKANALO KAMA “AMARULA PAN AFRICAPROMOTION”.

Meneja wa kinywaji cha Amarula Diana Baliagati
DAR ES SALAAM, Tanzania
KAMPUNI ya  Tanzania Distilleries Limited (TDL) leo imetangaza promosheni ya shindano la kumsaka mshindi wa anayetumia kinywaji cha Amarula, kinacho tengenezwa nchini Afrika Kusini na kusambazwa na TDL nchini maarufu kama nyumba ya Konyagi katika promosheni iliyozinduliwa leo Shoprite Mlimani City jijini Dar es Salam ijulikanayo kama  “Amarula Pan Africa Promotion”.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Bidhaa wa TDL, Diana Baliagati alisema shindano hili la kumsaka mtumiaji wa Amarula litaanza rasmi Desemba 16,2013 hadi Januari 14, 2014.

Diana alisema lengo hasa ikiwa ni kuwapa fursa wanywaji wa Amarula kwenda kutembelea nchi ya Afrika Kusini na kushuhudua shamba la Amarula na kujionea matunda ambayo hutumika kutengenezea kinywaji cha Amarula.

Mshindi katika shindano hili,atapata tiketi moja itakayomuwezesha kusafari na mwenzake kwa ajili ya kwenda kushuhudia shamba la AMARULA,nchini Afrika Kusini na kufikia katika Hoteli ya nyota tano(5Star), alisema Diana.

Meneja bidhaa wa TDL, Diana Baliagati alisema, ili kupata nafasi ya kujishindia tiketi,mshiriki anapashwa kujaza kuponi zilizo katika shingo ya chupa kubwa za Amarula zinazouzwa katika maduka makubwa yote ya Shoprite husika.Chupa hizo za shindano la Amarula Pan Africa Promotion zitakuwa zikipatika kwenye maduka ya Shoprite tu.

Mshindi wa Amarula Pan Africa Promotion atapatikana  kupitia droo itakayofanyika Januari 14,2014, na safari itakuwa mwezi Februari.Mshindi atapewa taarifa zote zinazohusika na safari  hiyo mara baada ya droo kufanyika

Monday, December 9, 2013

TBL YAPATA TUZO MBILI ZA UAJIRI BORA TANZANIA

 Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi cheti kwa Meneja Rasilimali Watu Uhusiano wa Kibiashara (HR Business Partner) wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Emmanuel Christopher (kulia), baada ya kampuni hiyo kupata tuzo ya utoaji mafunzo na maendeleo kwa wafanyakazi yakiwemo ya elimu ya jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Ukimwi. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bw. Almas Maige, Waziri wa Kazi na Ajira, Bi Gaudentia Kabaka na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO), Bw. Guy Ryder. Hafla hiyo ya kukabidhi tuzo kwa waajiri bora ilifanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Bi Gaudentia  akiipongeza TBL kupitia kwa Meneja Rasilimali Watu wa kampuni hiyo,Emmanuel Christopher
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO), Bw. Guy Ryder. akiipongeza TBL kupitia kwa Meneja Rasilimali Watu wa kampuni hiyo,Emmanuel Christopher

Monday, October 21, 2013

TAKWIMU KUHUSU PATO LA TAIFA



Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Wizara ya Fedha ina jukumu la kukokotoa Pato la Taifa kwa robo Mwaka ili kuwapatia takwimu  kwa wakati, wadau wa takwimu za Pato la Taifa katika vipindi vifupi vya robo mwaka ili kuweza kutathmini mabadiliko ya ukuaji wa uchumi.

Ukuaji halisi wa Pato la Taifa la Tanzania kwa bei za soko uliongezeka kwa kasi ya asilimia 6.7 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2013 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 6.4 katika kipindi kama hicho mwaka 2012. Jumla ya thamani ya Pato la Taifa katika kipindi husika ilikuwa Shilingi 5,012,935 milioni mwaka 2013 ikilinganishwa na Shilingi 4,699,884 milioni mwaka 2012.

Ukuaji wa Shughuli za Uchumi za Kilimo na Uvuvi
Shughuli za kiuchumi za kilimo zilifikia kasi ya ukuaji ya asilimia 5.3 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2013 zikilinganishwa na asilimia 5.1 ya robo kama hiyo mwaka 2012. Katika kipindi hicho, kulikuwa na mvua za kutosha katika mikoa inayozalisha mazao kwa wingi. Aidha, maelekezo ya ma-ofisa Ugani kwa wakulima kama kuchagua aina bora ya mbegu yalisaidia kuongeza uzalishaji.

Shughuli za uvuvi zilifikia kasi ya ukuaji wa asilimia 2.4 katika robo ya pili ya mwaka 2013 ikilinganishwa na asilimia 6.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2012. Kasi ya ukuaji huu ilipugua kutokana na kupungua kwa mavuno ya samaki kutoka kwenye maziwa, mito na mabwawa.

Shughuli za Uchumi za Viwanda na Ujenzi
Shughuli za uchimbaji madini, mawe na kokoto ziliongezeka kwa kasi ya asilimia 4.3 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2013 ikilinganishwa na kuporomoka kwa kasi ya ukuaji wa asilimia 5.1 katika kipindi kama hicho mwaka 2012. Kuongezeka kwa kasi hii ya ukuaji ilitokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa madini ya almasi na Tanzanite katika robo ya pili ya mwaka 2013.

Shughuli za uzalishaji bidhaa viwandani zilifikia kasi ya ukuaji ya asilimia 5.8 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2013 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 8.2 mwaka 2012. Kupungua kwa kasi ya ukuaji ya asilimia 2.4 (percentage point) kulitokana na kupungua kwa uzalishaji wa sementi, vyakula vilivyosindikwa na nguo.

Uzalishaji wa nishati ya umeme ulifikia kasi ya ukuaji wa asilimia 4.5 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2013 ikilinganishwa na kuporomoka kwa kasi ya ukuaji ya asilimia 1.1 katika kipindi kama hicho mwaka 2012. Kuongezeka kwa ukuaji wa nishati ya umeme kwa asilimia 5.6 (percentage point) kulitokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa nishati ya umeme unaotokana  na mafuta na gesi.

Ukuaji wa Shughuli za Uchumi za Utoaji Huduma
Shughuli za biashara za jumla na reja reja, ukarabati wa magari na pikipiki na vifaa vingine vya majumbani zilifikia kasi ya ukuaji wa asilimia 5.9 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2013 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 7.0 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2012. Kupungua kwa kasi kwa asilimia 1.1 (percentage point) kulitokana na kupungua kwa bidhaa zilizotengenezwa hapa nchini na zilizoagizwa kutoka nje ya nchi zilizouzwa katika kipindi hicho.  Shughuli za upangishaji nyumba, na shughuli zingine za biashara zilifikia kasi ya ukuaji wa asilimia 6.7.

Shughuli za uchukuzi na mawasiliano zilifikia kasi ya ukuaji wa asilimia 14.8 katika kipindi husika. Shughuli nyingine ni huduma za Hoteli na migahawa zilizofikia kasi ya ukuaji wa asilimia 3.2; Shughuli za uendeshaji Serikali zilifikia kasi ya asilimia 5.0, Elimu asilimia 5.7 na huduma za Afya na shughuli nyinginezo zilifikia kasi ya ukuaji wa asilimia 3.8 katika kipindi hicho.

Imetolewa na:
Morrice  Oyuke
Mkurugenzi wa Takwimu za Kiuchumi
Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Dar es Salaam

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu Takwimu za Pato la Taifa kwa robo ya pili ya mwaka 2013, wasiliana na  Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwenye anuani zifuatazo:

Mkurugenzi Mkuu,
Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
S.L.P. 796, Dar es Salaam.

Simu: +255 22 212 2722/3/4
Nukushi: +255 22 2130852
Barua pepe: dg@nbs.go.tz  Tovuti:www.nbs.go.tz

Monday, October 14, 2013

MAGAUNI NA VIPODOZI KUTOKA MAREKANI VYAWASILI DAR

flyer-to-blogs   Bringing you fashionable designer office wear (calvin klein, Tahari etc) at an affordable price. Everything is 120,000 and 60,000tshs ONLY. Original MAC Lipstick for TSH 50, 000 ONLY Victoria Secret LipGlossy for TSH 25,000 ONLY

Wednesday, October 9, 2013

TPB YATANGAZA WASHINDI DROO YA MWISHO YA SHEREHEKEA MSIMU WA IDDI NA TPB WESTERN UNION

IMG_0159  
Meneja Mkuu Uendeshaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Kolimba Tawa (kulia) akimsoma mmoja wa washindi wa shindano la Sherehekea Msimu wa Iddi na TPB Western Union leo jijini Dar es Salaam.
IMG_0134  
Meneja Mkuu Uendeshaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Kolimba Tawa (wa pili kulia) akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa shindano la Sherehekea Msimu wa Iddi na TPB Western Union leo jijini Dar es Salaam akimjulisha ushindi wake.
IMG_0101  
Mmoja wa vijana maalumu akikabidhi moja ya kuponi baada ya kuitoa kwenye boksi ili kumpata mmoja wa washindi wa shindano la Sherehekea Msimu wa Iddi na TPB Western Union.
IMG_0092  
Mmoja wa vijana maalumu wakichanganya kuponi kwenye boksi kabla ya kuchagua moja wapo ili kumpata mshindi wa shindano la Sherehekea Msimu wa Iddi na TPB Western Union.
Na Joachim Mushi, Dar
  BENKI ya Posta Tanzania (TPB) hatimaye leo imewataja washindi wa droo ya mwisho wa Shindano la Sherehekea Msimu wa Iddi na TPB Western Union lililokuwa likiendeshwa na benki hiyo. Akizungumza katika hafla fupi na wanahabari jijini Dar es Salaam ya kuwataja washindi hao nane, Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa alisema zoezi hilo ni mwendelezo wa benki hiyo katika kurejesha sehemu ya mapato ya benki kwa wateja wake. Alisema washindi hao nane kwa jumla wamejishindia shilingi milioni 1.5. Akifafanua zaidi alisema mshindi wa kwanza ambaye ni Elias Mwalamala kutoka Dar es Salaam amejishindia sh. 500,000/-, na mshindi wa pili, Nathan Gawangi kutoka Kigoma akijipatia kitita cha sh. 300,000/-, huku mshindi wa tatu Bruno Hindu (Dar es Salaam) akifanikiwa kuibuka na sh. 200,000/-. Alisema washindi wengine watano ambao nao benki hiyo itawazawadia sh. 100,000/- kila mmoja ni pamoja na Miss Farida kutoka Zanzibar, Alfa Mwakalinga wa Dodoma, Mariam Mtungo, Ramadhan Mapuya kutoka pamoja na Fadhili Daud Mbaga wote kutoka Dar es Salaam. Aidha Tawa aliongeza kuwa washindi wote watapigiwa simu na uongozi wa TPB na kuelekezwa namna ya kupata zawadi zao waliojishindia wakiwa ni miongoni mwa wateja waliotuma na kupokea fedha kupitia huduma ya Western Union. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

Tuesday, September 17, 2013

HOTELI YA DOUBLETREE YAGAWA TAA ZA UMEME JUA ZENYE THAMANI YA TSH 5MILLIONI VISIWANI

Fundo 2
Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata akiwaelekeza wanafunzi wa shule ya Msingi Maskul Fundo, Jimbo la Gando kisiwani Pemba jinsi ya kutumia taa za nishati Jua walipotembelea shule hiyo katika moja ya kampeni zake za kugawa taa za nishati mbadala kwa shule za msingi nchini.
Fundo 3
Mkurugenzi wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann akiangalia jinsi mwanafunzi anavyoweza kuwasha taa ya nishati ya Umeme Jua jana visiwani katika jimbo la Gando.
Fundo 1
Wanafunzi wa shule ya Msingi Maskul Fundo, Jimbo la Gando kisiwani Pemba wakiwa wamepozi kwenye picha ya pamoja wakati wa hafla ya kukabidhiwa taa za nishati ya Umeme Jua zilizotolewa na Hoteli ya DoubleTree.
. Ni muendelezo wa kampeni ya nishati ya mbadala
.Lengo ni kusaidia wananchi kuelewa matumizi ya Umeme Jua ambao ni rafiki wa mazingira
.Ni programu ya miaka miwili mashuleni
Na Damas Makangale, Moblog
Hoteli ya Double Tree by Hilton ya jijini Dar es Salaam imeendelea na kampeni zake kabambe ya matumizi ya nishati ya jua kwa kugawa taa 200 kwenye shule ya Msingi Maskul Fundo, Jimbo la Gando kisiwani Pemba, Moblog linaripoti.
Akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ya kugawa taa hizo jana, Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Ndugu Said Ali Mbarouk ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Gando, amesema kwamba msaada huo wa Double Tree kwa shule hiyo ni kielelezo tosha kwamba sekta binafsi zina mchango mkubwa katika sekta ya elimu hapa nchini.
“Napenda kuchukua fursa hii adhimu kuwashukuru uongozi na wafanyakazi wote wa Double Tree kwa msaada wao mkubwa kwa shule yetu ya hapa Gando ambapo watoto wetu watasoma katika mazingira rafiki yatayowawezesha kufaulu mitihani yao,’ alisema Mbarouk.
Waziri Mbarouk amesema kwamba kutokana na mabadiliko ya tabia nchi Serikali, wananchi na wadau wote wa maendeleo hawawezi kuendelea kutegemea umeme wa vyanzo vya maji na badala yake umeme wa jua ambao ni nishati mbadala ni ufumbuzi wa tatizo la nishati nchini.
Amesema mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi hasa kwenye nishati ni muhimu kwa sababu ni nishati ndio injini ya Uchumi wa taifa lolote lile hapa duniani kwa sasa.
‘lakini kampeni hizi zitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi kutambua na kuelewa nishati mbadala na umuhimu wake katika maisha ya kila siku ikiwemo mazingira,” alisisitiza
Hoteli ya DoubleTree ilizindua rasmi kampeni ya matumizi ya nishati ya jua ambayo itadumu kwa muda wa miaka miwili katika shule za msingi nchi nzima miezi kadhaa iliyopita.
DoubleTree itakuwa ikigawa taa 200 za mezani zenye kutumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa shule tofauti kila mwezi, lengo likiwa nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira kwa kupitia mafunzo katika madarasa yao.

Monday, August 19, 2013

TBL YAZINDUA KAMPENI YA NYUMBANI NI NYUMBANI YA GRAND MATL NA VITA MALT



Meneja mahusiano wa TBL Doris Malulu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya uzinduzi wa kampeni kubwa ya vinywaji hivyo kuwatembelea watumiaji majumbani mwao na kutoa elimu juu ya umuhimu wa kutumia vinywaji vilivyo bora , Kampeni hiyo itajulikana kwa jina la Nyumbani ni Nyumbani na itajumuisha mikoa kumi ya Tanzania Bara,Kulia ni meneja wa vinywaji hivyo Consolata Adam.
Na Mwandishi Wetu
KATIKA kile kinachoonekana kusogeza huduma bora zaidi kwa wananchi na kutambua umuhimu wa afya zao, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia vinywaji vya Grand Malt na Vita Malt imezindua kampeni maalumu iitwayo ‘Nyumbani Ni Nyumbani’ kwa ajili ya kupeleka bidhaa hizo zisizo na kilevi kwa Watanzania wote.

Akizindua kampeni jijini Dar es Salaam jana, Meneja Bidhaa zisizo na vileo wa TBL, Consolata Adam alisema, wamezindua kampeni hiyo maalumu ili kuhakikisha vinywaji visivyo na kilevi vinamfikia kila mtu.

“Tumeamua kuzindua kampeni hii ili kuhakikisha kila Mtanzania anafahamu umuhimu wa vinywaji vya Grandmalt na Vitamalt katika matumizi ya kutunza na kulinda afya zao.

“Kampeni hii itahusisha mabalozi wa Grand Malt na Vita Malt kwa pamoja kutembea nyumba kwa nyumba na kuhakikisha ujumbe huu unamfikia kila mtu katika nyumba yake ambapo pia kutakuwa na fursa ya kujishindia na kuzawadiwa zawadi mbalimbali wakati wa kampeni hiyo,” alisema.

Consolata alisema, vinywaji hivyo ni vizuri zaidi kwa afya ya mwanadamu kwani vimet engenezwa vikiwa na virutubisho vya kila aina na vinafaa mno hata kwa mama mjamzito.

“Tunaomba Watanzania wasishangae pale watakapokutana na watu wetu ambao watakuwa wanawatembelea majumbani kwao, kwani lengo ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata fursa ya kutambua faida za kutumia kinywaji cha Grand Malt  na Vita Malt katika kulinda afya yake ili tuweze kujenga desturi ya kuwa na matumizi bora kwa ajili ya kujenga afya zetu,” alisema.

Nayee Afisa Uhusiano wa TBL, Doris Malulu alisema hii ni kampeni ya kwanza kuzinduliwa na vinywaji hivyo kwa lengo moja la kuwawezesha Watanzania kutumia bidhaa hizo zenye faida kubwa kwa mwili wa mwanadamu.

“Tunataka bvinywaji hivi vipatikane kila mahali na pia kuwasaidia Watanzania umuhimu wa kuvitumia kwani vina faida kubwa kwa wote, kuanzia hata kwa mtoto,” alisema Doris.

Kampeni hiyo ya ‘Nyumbanio ni Nyumbani’ inatarajiwa kuanza katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Mtwara, Dodoma, Iringa, Morogoro, Mbeya na Shinyanga ambapo itaanzia mji wa Kahama.


Vinywaji vya Grand Malt na Vita Malt ambavyo havina kilevi vinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Sunday, August 18, 2013

WABUNGE: SERIKALI ITUMIE RISITI ZA ELEKTONIKI


BY ZITTO KABWE
Major  Highlights
1.) Kutokana na kutokuwepo na taarifa sahihi kuhusu deni la Taifa kuna umuhimu wa kukutanisha wadau wakuu wanaohusika hususani BOT, HAZINA, Kamati za Bunge na CAG ili kuweza kujua kwa usahihi zaidi ukubwa wa deni hilo.  Vile vile imeamuliwa kuwa Serikali ishauriwe kuunda chombo huru kitakachosimamia deni la taifa.
2.) Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma haiweki uwazi wa kutangaza umiliki wa mali za viongozi.  Hii inapelekea viongozi kutoweka wazi mali wanazomiliki na ni rahisi mtu kuzushiwa umiliki usio wa ukweli.  Ni vyema Sekretarieti wakafanya utafiti wa umiliki wa mali kwa viongozi wa Umma na kuweka taarifa hizo katika tovuti ya Sekretariati ili kuwawezesha wananchi kuweza kuona mali zinazomilikiwa na viongozi wao; na pale ambapo kiongozi hatakuwa ametoa taarifa ya umiliki huo basi taarifa hiyo itolewe kwa Tume.
3.) Kwa kuwa leseni za udereva za sasa zinaweza kuweka kumbukumbu za makosa ya usalama barabarani, basi TRA ikishirikiana na  Wizara ya Mambo ya Ndani zihakikishe ya kuwa Askari wa Usalama Barabarani wanatumia utaratibu huu wa kisasa wa kutoa  “notification” na kutoa risiti za malipo za elektroniki.
4.) Maduhuli ya Serikali sasa yakusanywe kwa kutumia risiti za elektroniki.  Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma yaanze kutumia risiti za eletroniki mara moja ili kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali yanayotokea hivi sasa katika kutumia risiti zinazoandikwa kwa mkono. Pia ofisi za serikali zifanye manunuzi yake kwa wafanyabiashara wanaotumia mashine za kielektroniki.
5.) “The Proceeds of Crime Act, 1991” ifanyiwe marekebisho na kuweka kifungu kinachomwezesha AG/DPP kuwa na mamlaka ya kuomba mahakama kufungua kesi ya madai (Civil Forfeiture) kwa watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Friday, August 2, 2013

ADV/TANGAZO

MAYFAIR HOTEL

Suites | Conferences | Events

  • Free high-speed wireless Internet Access
  • A Kitchenette with Microwave, Refrigerator, etc.
  • A nice small coffee table with four charis, gives you feel like at home
  • A spacious nice Bathroom with bath tub and hair-dryer, etc.
Contact Details:
Mobile: +255 685-688000
Email: info@mayfairplaza.com
Website: 
www.mayfairhoteltz.com
Address: Mayfair Hotel, Old Bagamoyo Road, Dar es Salaam, Tanzania.

123Tanzania E-Shots
 
27,000+ Subscribers all over the Tanzania.
123Tanzania.com is the largest B2B online directory of Tanzania with more than15,000 monthly visitors

Contact Us: English or Kiswahili +255 773 858 090, +255 22 213 3039

Copyright © 2013 123Tanzania, All rights reserved. 
You are receiving this email from 123tanzania.com, Tanzania's largest Business portal. If you would like to unsubscribe from this list, simply click unsubscribe from the link below. Please note: unsubscribing from this list will only unsubscribe you from Newsletters E-Shots, it will not unsubscribe you from the Promo E-Shots. 

Our mailing address is: 
123Tanzania
Elia Complex
Zanaki Street
Dar Es Salaam 8758
Tanzania

Thursday, August 1, 2013

WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA TBL MBEYA



Waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya wakitembelea kapuni ya Bia TBL
Moja ya watumishi wa kampuni hiyo ya Bia akiwaeleza waandishi wa habari jinsi bia inavyotengenezwa
Ziara inaendelea

Meneja kiwandacha kampuni ya Bia TBL  Mbeya Nicolaus  Kanyamala akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kiwanda hicho
Baadhi ya wa watumishi wa kampuni ya Bia wakijitambulisha mbele ya waandishi wa habari


Meneja uhusiano wa TBL Dorris Malulu akizungumza na waandishi wa habari
Meneja masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Kanda ya Mbeya, Raymond  Degera, akielezea mafanikio ya kampuni ya Bia
Mpishi Mkuu wa Bia wa Kampuni ya Tbl, Tito alisema Sheria za Tanzania zinatakiwa kusimamiwa ipasavyo kuhusu matumizi ya Vilevi kwa kuwashtaki wanaozidisha pombe na wengine wanaokunywa mida ya kazi na kuleta usumbufu kwa wengine.
Wanahabari walipata fursa ya kuelezwa sheria za
unywaji wa Pombe na madhara yake, umri wa mtu kuanza kunywa pombe pamoja na
madhara yake ambapo baada ya zoezi hilo walitembelea maeneo mbali mbali ya
Kiwanda hicho.
Baada ya kutembelea kiwanda  sasa ilifika wakati wa kuonja Bia na kuitambua radha yake
Unaonja na kutaja ni bia gani kama ni NDOVU au KILIMANJARO kunaalama za rangi zimewekwa katika grass
Mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango akionja na kujaza katika fomu kuwa hiyo aliyoinja ni Bia gani
 Meneja
kiwanda cha kampuni ya Bia TBL  Mbeya Nicolaus  Kanyamala akimkabidhi
zawadi Joseph mwaisango mara baada ya kuibuka mshindi wa uwonjaji bia
 Meneja
kiwanda cha kampuni ya Bia TBL  Mbeya Nicolaus  Kanyamala akimkabidhi
zawadi Emmanuel Madafa baada ya kushinda uonjaji wa Bia
Mshindi wa pili Joachim Nyambo akipokea zawadi yake toka kwa meneja wa kampuni ya bia 
Picha ya pamoja



ZAIDI ya Tani 60,000 za Shayiri zinatarajiwa kuvunwa kutoka kwa Wakulima wa  Kanda ya Nyanda za Juu Kusini baada ya kupatiwa mafunzo juu ya kilimo cha mazao yenye tija na uwepo wa soko la uhakika. Aidha zaidi ya Wakulima 400 kutoka Kanda hiyo ndiyo walionufaika na Kilimo hicho na kujihakikishia Soko la zao ambalo hutumika zaidi katika utengenezaji wa Vinywaji moto ambavyo ni Bia na

uzalishaji mwingine kutokana na uwepo wa Viwanda vikubwa vya kuzalisha Vinywaji hivyo.


Hayo yalibainishwa juzi na Meneja masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Kanda ya Mbeya, Raymond  Degera,wakati wa Ziara ya Waandishi wa Habari katika Kiwanda cha Bia kilichopo Iyunga Jijini Mbeya.


Alisema  kutokana na uwepo wa Kiwanda cha Bia Mkoani Mbeya na kuhudumia Wananchi wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini waliona si vema Malighafi zikatoka Nje ya Mikoa hiyo ili hali ardhi na hali ya Hewa inaruhusu kilimo cha mazao hayo na kuamua kutoa elimu namna ya kunufaika na Kilimo.


Degera alisema Kampuni  ilianzisha Programu ya kuwawezesha Wakulima kuhusu kilimo cha mazao yenye tija ambapo Wakulima wa Wilaya ya Mbozi,

Sumbawanga na Iringa wanaofikia 400 ambao waliitikia na kuanza uzalishaji ambao baada ya mavuno kiwanda kitanunua moja kwa moja kutoka kwa wakulima ambao wanatarajia kuvuna Tani 60,000.


Kwa upande wake  Mpishi Mkuu wa Bia wa Kampuni ya Tbl, Tito alisema Sheria za Tanzania zinatakiwa kusimamiwa ipasavyo kuhusu matumizi ya Vilevi kwa kuwashtaki wanaozidisha pombe na wengine wanaokunywa mida ya kazi na kuleta usumbufu kwa wengine.


Alisema Utaratibu wa Nchi zingine huwalazimisha wananchi wake kutumia Chupa mbili za Bia kwa siku na kwamba anayehitaji kuongeza zaidi ya hapo wauzaji huwakatalia, Sheria ambayo alishauri kutumika ili kuongeza uzalishaji na kuiondoa nchi katika majanga yanayotokana na ushawishi wa Pombe.


Aliongeza kuwa  kama wamiliki na watengenezaji wa Pombe wanahitaji wananchi wanywe kwa utaratibu ili waendelee kuwa wateja wao na  kusaidia kuchangia kodi kwa Taifa kutokana na Kampuni hiyo kuongoza kwa kuchangia kodi katika pato la Taifa.


Aidha katika Ziara hiyo Wanahabari walipata fursa ya kuelezwa sheria za unywaji wa Pombe na madhara yake, umri wa mtu kuanza kunywa pombe pamoja na madhara yake ambapo baada ya zoezi hilo walitembelea maeneo mbali mbali ya Kiwanda hicho.


Mbali na hilo wanahabari hao pia walishindanishwa kuonja Bia na kuzitambua kwa majina zoezi ambalo lilikuwa gumu kwa waandishi wengi huku Waandishi wanne wakiibuka washindi baada ya wawili kushika nafasi ya kuanza kwa kupata alama tatu kati ya Tano ambao ni Emmanuel Madafa na Joseph Mwaisango huku alioshika nafasi ya pili kwa kupata alama mbili kwa tano wakiwa ni Joachim Nyambo na Kenneth Ngelesi.