Picha ya pamoja
ZAIDI ya Tani 60,000 za Shayiri zinatarajiwa kuvunwa kutoka kwa Wakulima wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini baada ya kupatiwa mafunzo juu ya kilimo cha mazao yenye tija na uwepo wa soko la uhakika. Aidha zaidi ya Wakulima 400 kutoka Kanda hiyo ndiyo walionufaika na Kilimo hicho na kujihakikishia Soko la zao ambalo hutumika zaidi katika utengenezaji wa Vinywaji moto ambavyo ni Bia na
uzalishaji mwingine kutokana na uwepo wa Viwanda vikubwa vya kuzalisha Vinywaji hivyo.
Hayo yalibainishwa juzi na Meneja masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Kanda ya Mbeya, Raymond Degera,wakati wa Ziara ya Waandishi wa Habari katika Kiwanda cha Bia kilichopo Iyunga Jijini Mbeya.
Alisema kutokana na uwepo wa Kiwanda cha Bia Mkoani Mbeya na kuhudumia Wananchi wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini waliona si vema Malighafi zikatoka Nje ya Mikoa hiyo ili hali ardhi na hali ya Hewa inaruhusu kilimo cha mazao hayo na kuamua kutoa elimu namna ya kunufaika na Kilimo.
Degera alisema Kampuni ilianzisha Programu ya kuwawezesha Wakulima kuhusu kilimo cha mazao yenye tija ambapo Wakulima wa Wilaya ya Mbozi,
Sumbawanga na Iringa wanaofikia 400 ambao waliitikia na kuanza uzalishaji ambao baada ya mavuno kiwanda kitanunua moja kwa moja kutoka kwa wakulima ambao wanatarajia kuvuna Tani 60,000.
Kwa upande wake Mpishi Mkuu wa Bia wa Kampuni ya Tbl, Tito alisema Sheria za Tanzania zinatakiwa kusimamiwa ipasavyo kuhusu matumizi ya Vilevi kwa kuwashtaki wanaozidisha pombe na wengine wanaokunywa mida ya kazi na kuleta usumbufu kwa wengine.
Alisema Utaratibu wa Nchi zingine huwalazimisha wananchi wake kutumia Chupa mbili za Bia kwa siku na kwamba anayehitaji kuongeza zaidi ya hapo wauzaji huwakatalia, Sheria ambayo alishauri kutumika ili kuongeza uzalishaji na kuiondoa nchi katika majanga yanayotokana na ushawishi wa Pombe.
Aliongeza kuwa kama wamiliki na watengenezaji wa Pombe wanahitaji wananchi wanywe kwa utaratibu ili waendelee kuwa wateja wao na kusaidia kuchangia kodi kwa Taifa kutokana na Kampuni hiyo kuongoza kwa kuchangia kodi katika pato la Taifa.
Aidha katika Ziara hiyo Wanahabari walipata fursa ya kuelezwa sheria za unywaji wa Pombe na madhara yake, umri wa mtu kuanza kunywa pombe pamoja na madhara yake ambapo baada ya zoezi hilo walitembelea maeneo mbali mbali ya Kiwanda hicho.
Mbali na hilo wanahabari hao pia walishindanishwa kuonja Bia na kuzitambua kwa majina zoezi ambalo lilikuwa gumu kwa waandishi wengi huku Waandishi wanne wakiibuka washindi baada ya wawili kushika nafasi ya kuanza kwa kupata alama tatu kati ya Tano ambao ni Emmanuel Madafa na Joseph Mwaisango huku alioshika nafasi ya pili kwa kupata alama mbili kwa tano wakiwa ni Joachim Nyambo na Kenneth Ngelesi.
|
0 comments:
Post a Comment