Monday, March 20, 2017

AIRTEL KUZINDUA MADUKA ZAIDI YA 2000 TANZANIA

·        Wateja wa Airtel kupata huduma kwa haraka na karibu zaidi
·        Mradi huu utachochea upatikanaji wa huduma za kifedha
·        Airtel yaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuendelea kuwekeza nchini
Shinyanga 
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imetangaza mpango wake wa kuzindua ma duka Saidi ya 2000 nchini utakaowawezesha wateja wake  kupata huduma na bidhaa zake za kibunifu kwa urahisi zaidi

maduka haya ya Airtel yatakuwa na muonekano unaofanana na yatakuwa katika maeneo maalumu ambayo yatawawezesha maelfu ya wakazi kupata huduma kirahisi na kukidhi mahitaji yao kwa ufanisi zaidi

Maduka hayo yatatoa huduma mbalimbali zikiwemo huduma za kifedha, huduma za intaneti, kuongeza salio , kusajili namba na pia kuunganisha wateja wapya kwenye mtandao wa Airtel

Katika kutekeleza mpango huo wa Airtel imezindua maduka 8 katika mkoa wa Shinyanga kwenye uzinduzi uliofanywa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel ambapo Airtel imeeleza mpango wake wa kujitanua zaidi na ili kufikisha huduma zake karibu na watanzania waishio mjini na pembezoni ya nchi

Akiongea wakati wa uzinduzi maduka hayo mkoani Shinyanga, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bwn Sunil Colaso alisema” tunajisikia fahari kutangaza azma yetu kubwa itakayowezesha upatikanaji wa bidhaa na huduma zetu kirahisi zaidi na kuendelea kuthibitisha dhamira yetu ya kuwapatia wateja wetu huduma bora. leo tunazindua maduka 8 hapa shinyanga na mpango wetu ni kuwa na jumla ya maduka yapatayo 76 mkoani hapa

Tunaamini hii ni njia pekee ya kuwafikia wateja wetu kujua changamoto zao na kuzitatua kwa wakati na vilevile kuwaunganisha na huduma na bidhaa zetu za kipekee na kibunifu zinazosaidia kutatua changamoto zao za kila siku za kijamii na kiuchumi. Mpango wetu ni kuwa na maduka kama haya takribani 2000 nchi nzima na tayari tumeshaanza kufungua maduka haya kwa kasi katika maeneo mbalimbali nchini. Aliongeza Colaso

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi Josephine Matiro alisema” Tunafurahi kuona juhudi zinazofanywa na Airtel katika kusogeza huduma zake na wateja wake lakini  pia kutengeneza ajira kwa wengi. Tunaamini maduka yanayozinduliwa leo hapa Shinyanga na yale yatakayozinduliwa mbeleni yatachochea kwa kasi kwa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi kwa urahisi na kwa usalama na kutoa mwanya kwa Maendeleo Mengi kuku a kiuchumi. Napenda kuwahamasisha wamiliki wa maduka kutumia fursa hii kutanua biashara zenu na kutengeneza ajira kwa vijana hapa mkoani Shinyanga.


Kuanzishwa kwa maduka haya sehemu mbalimbali nchini kunathibitisha kwa vitengo dhamira ya Airtel kuendelea kuwekeza nchini na Afrika kwa ujumla
 Meneja  Mauzo wa Airtel Shinyanga, James Moilo (kushoto) akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga , Josephine Matiro  moja kati ya simu za Smartphone zinazopatikana katika moja kati ya maduka wakati Airtel ilipozindua duka la huduma kwa wateja mkoani Shinyanga. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Bwn Sunil Collaso

 Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Bwn Sunil Collaso akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga , Josephine Matiro  kabla ya uzinduzi wa duka mkoani hapo
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga , Josephine Matiro  akiwapongeza wa Airtel kwa kuuanzisha mpango wa kufungua maduka zaidi ya 76 na kufikisha huduma kwa wateja kwa urahisi mkoani shinyanga

0 comments:

Post a Comment