Sunday, July 2, 2017

MAMLAKA YA UDHIBITI WA UNUNUZI KATIKA SEKTA YA UMMA (PPRA) KATIKA MAONESHO YA SABASABA 2017

Meneja Usimamizi na Utawala waMifumo ya TEHAMA, wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi katika Sekta ya Umma (PPRA), Bw.Bernard Ntelya, (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensehni wa PPF, Bw. William Erio, alipotembeela banda la Mamlaka hiyo Julai 2, 2017.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi katika Sekta ya Umma, (PPRA), kama zilivyo taasisi nyingine za serikali, imeweka banda lake kwenye jingo la Wizara ya Fedha na Mipango, wakatihuuwa maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Viongozi na maafisa wa juu wa serikali wamepata fursa ya kutembelea banda hilo ili kujua huduma wanazotoa kwenye banda hilo, ambapo maafisa wa PPRA, wamekuwa wakitoa elimu na kugawa vipeperushi vyenye maeelzo mbalimbali ya kazi za Mamlaka hiyo, lakini na taarifa zinazoeleza sheria ya manunuzi ya umma na umuhimu wake.

Mamlaka hiyo imeanzishwa kwa sheria ya manunuzi ya Umma CAP 410 kama ilivyobadilishwa na Sheria ya Manunuzi ya Umma ya namba 7 ya mwaka 2011 ambayo inatoa Mamlaka ya kusimamia manunuzi ya umma kwa taasisi zote za Umma (Serikali), upande wa Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa maafisa wa PPRA walioko kwenye banda hilo, wanasema, malengo makuu ya PPRA ni kuhakikisha manunuzi yote kwenye taasisi za umma, yanafanyika kwa usawa katika shindani, uwazi, bila unyanyasaji ili mwisho wa siku watoa huduma watoe huduma inayolingana na thamani ya fedha wanazolipwa kwa maendeleo ya taifa, (Value for Money).

Aidha wamesema, PPRA inao wajib u wa kuweka viwango katika mfumo wa manunuzi ya umma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (upande wa Tanzanai Bara).


Afisa Mwandamizi wa PPRA, Bw. Mcharo Mrutu, (kulia), akimpatia vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali za PPRA, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio
Bw. Mrutu, (kulia), akizungumza na Mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mamlaka hiyo
Bw. Ntelya(kulia), akifafanua jambo kwa mwananchi huyu aliyefika kujua shughuli za PPRA

0 comments:

Post a Comment