This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Friday, December 30, 2016

MAONI YA WATEJA NI MUHIMU KWA UKUAJI WA BIASHARA YAKO

Na Jumia Travel Tanzania
KUJA kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia hususani mtandao wa intaneti kumebadilisha kwa kiasi kikubwa mienendo ya matangazo ya utoaji wa huduma mbalimbali duniani na hii ni kutokana na uwezo wake wa kuwaruhusu wateja kutoa ushuhuda, kukosoa au kutoa maoni juu ya walichohudumiwa na kujionea.

Tofauti na kipindi cha nyuma kidogo ambapo wataalamu wa masoko walikuwa wanatumia zaidi njia za luninga na redio kuwafikia wateja wao, siku hizi mfumo wa intaneti unapewa kipaumbele zaidi kutokana na namna unavyofikia watu wengi zaidi ndani ya muda mfupi, kwa haraka na gharama kidogo.

Matangazo ya luninga na redio yanaweza kuwa hayana ushawishi mkubwa ukilinganisha na mtandao wa intaneti kwani hivi sasa makampuni yanaweza kuwasilisha bidhaa na huduma zao na kupokea majibu kujua kwamba zinakubalika au la. Hali hiyo ni dhahiri kutokana na makampuni mengi kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika teknolojia na rasilimali watu katika kusimamia tovuti na kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter, instagram na mingineyo.

Kupitia tovuti na kurasa hizo za mitandao ya kijamii biashara na huduma nyingi zinafanya vizuri kutokana na ushawishi wao kwenye mitandao kutokana na namna ambavyo zinazungumziwa vizuri na watu wengi. Lakini pia husaidia kampuni hizo husika kuwasiliana moja kwa moja na wateja wao kwa sababu wateja huwasilisha maoni yao moja kwa moja mtandaoni tofauti na luninga au redio ambazo hutoa fursa ya kuona au kusikiliza tu matangazo.

Vivyo hivyo hali hii inaweza kusaidia sana ukuaji wa sekta ya utalii na ukarimu kama vile huduma za hoteli na malazi ambazo hujitangaza zaidi kupitia namna wateja wanavyozizungumzia

Jumia Travel (www.travel.jumia.com) kampuni unaongoza kwa huduma za hoteli mtandaoni barani Afrika umezitunuku vyeti hoteli kadhaa ambazo zilizopendekezwa na kutembelewa ndani ya wateja wengi kipindi cha mwaka mzima wa 2016.

Akizungumzia juu ya umuhimu wa vyeti hivyo Meneja Mkazi wa Jumia Travel Tanzania, Bi. Fatema Dharsee amesema kuwa, “Vyeti hivi vina umuhimu mkubwa kwani ni viashiria vikubwa vya namna hoteli yako inatathminiwa vipi na wateja pindi wanapoitembelea. Siku zote wateja huambizana huduma wanazozipata sehemu za biashara wanazotembelea na kutokana na ushuhuda huo ndio na wengine hushawishika kutembelea pia. Kupitia mtandao wetu wateja wanayofursa ya kutoa maoni juu ya hoteli walizozitembelea, huduma walizopatiwa, mapungufu waliyoyaona na maboresho ambayo wangependa yafanyiwe kazi.”

“Imefikia mahala sasa ni lazima wataalamu wa masoko watambue mchango na ushawishi walionao wateja kwenye kukua kwa biashara zao kwani nguvu yao ni kubwa zaidi ya matangazo wanayoyalipia kupitia luninga na redio au njia nyinginezo. Maneno au ushuhuda unaotolewa na wateja unatosha kwa kiasi kikubwa mtu kutumia bidhaa au huduma yako kwani ni halisi kutokana na mtu kuitumia au kupatiwa huduma hiyo husika. Hivyo ningependa kutumia fursa hii kuwataka mameneja wa hoteli waliokabidhiwa vyeti hivi kuichukulia hali hii kama ni changamoto kwao kwa kufuatilia maoni ya wateja yanayoachwa kwa njia ya mtandao na kuyafanyia kazi.” Alihitimisha Bi. Dharsee.

Hoteli ambazo zimepatiwa vyeti hivyo ni pamoja na Jafferji House & Spa Hotel na Garden Lodge za visiwani Zanzibar, Golden Tulip Hotel, Peacock Hotel na Butterfly Hotel zote za jijini Dar es Salaam.

EWURA YARIDHIA KWA SEHEMU OMBI LA TANESCO KUPANDISHA BEI YA UMEMEMAMLAKA ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA), imetangaza ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 8.5%.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlamgosi, (pichani), ongezeko hilo la bei ni kufuatia maombi ya Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), ambalo liliwasilisha maombi EWURA ya kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19, ifikapo Januari mwaka 2017.

Akitangaza bei hizo mpya jijini Dar es Salaam, leo Mkurugenzi Mkuu huyo wa EWURA amesema, baada ya kufanya uchambuzi wa kina, Mamlaka yake imefikia uamuzi wa kuongeza asilimia 8.5 itakayoanza kutumika Januari Mosi, 2017 kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wake.

Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa kwa asilimia 5.7% ya bei ya umeme.

Hata hivyo ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao hayazidi uniti 75 kwa mwezi.

Kundi la TIB linalohusisha viwanda vidogo, mabango na minara ya mawasiliano litakua na tozo ya mwezi ya shilingi 5,520.

Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), linaendelea kufanya maboresho ya miundombinu ya umeme na kutekeleza miradi mipya ya kuunganisha wateja ili kuboresha huduma za umeme nchini.

Wednesday, December 28, 2016

DSTv WAMPA SHAVU MWANDISHI MO BLOG

Kampuni ya Multichoice Tanzania wasambazaji wa visambuzi vya kisasa vya DSTV mapema leo 28 Desemba 2016, wametoa zawadi ya msimu wa Sikukuu kwa wadau wao mbalimbali ikiwemo kwa mwandishi Mwandamizi wa mtandao (Blog) wa MODEWJIBLOG, Ndugu Andrew Chale. Akikabidhi zawadi kwa niaba ya uongozi wa kampuni hiyo ya Multichoice Tanzania, Costomer Retention Representative, Vida Msuya aliipongeza MO BLOG na mwanahabari huyo kwa kuwa mstari wa mbele katika kuitangaza vyema DSTV kwa muda wote na zawadi hiyo ni moja ya kurudisha fadhila kwa wadau wao. “Lengo la DST ni kuona tunazidi kuwa na wateja wengi ambao pia wanapata kitu bora kutoka kwetu. Huduma zetu nzuri na za kisasa hivyo kwa msimu huu wa Sikukuu wateja wetu na wadau tunawatembea na kuwapatia zawadi.” Alieleza Vida Msuya. Aidha, DSTV pia imeweza kuwapatia wadau mbalimbali zawadi hizo za Sikuukuu na kuwatakia kheri ya Mwaka mpya wa 2017. Aidha, kupitia kwa Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Bw. Alpha Joseph hivi karibuni amebainisha kuwa katika msimu huu wa kusherehekea Sikukuu ya krismas na mwaka mpya wateja wao watapata kuangalia chaneli zaidi ya 70 za DStv ikiwemo mpira wa ligi ya Hispania (Laliga) na ligi ya Uingereza na zingine nyingi huku wakishusha bei za vifurushi vyao kwa wastani wa asilimia 16, kifurushi maarufu cha DStv Bomba chenye chaneli zaidi ya 70 kikipunguzwa bei hadi sh.19,975 tu kwa mwezi. DSTV
Customer Retention Representative wa DStv, Vida Msuya (kulia) akimkabidhi zawadi ya msimu wa Sikukuu ya Chris Mass na Mwaka Mpya kwa mwandishi Mwandamizi wa mtandao wa MO BLOG, Bw. Andrew Chale katika ofisi za mtandao huo Jijini Dar es Salaam. Zawadi hiyo kutoka kwa kampuni ya Multichoice Tanzania.
dstv-andrew
Customer Retention Representative wa DStv, Vida Msuya na Mwandishi Mwandamizi wa mtandao wa MO BLOG, Bw. Andrew Chale wakiwa na zawadi hiyo wakati wa kukabidhi.
DSTV NA ANDREW CHALE
Customer Retention Representative wa DStv, Vida Msuya (kulia) akimkabidhi zawadi ya msimu wa Sikukuu ya Chris Mass na Mwaka Mpya kwa mwandishi Mwandamizi wa mtandao wa MO BLOG, Bw. Andrew Chale katika ofisi za mtandao huo Jijini Dar es Salaam. Zawadi hiyo kutoka kwa kampuni ya Multichoice Tanzania.

Friday, March 11, 2016

DROO YA PILI PROMOSHENI YA "JAZA MAFUTA NA USHINDE" KUTOKA GAPCO YAFANYIKA LEO

Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO, Rashid Khalfan (kulia) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya pili ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" inayoendeshwa na Kampuni hiyo na kusimamiwa na Mkaguzi wa Michezo ya kubahatisha nchini, Abdallah Hemedy (kushoto). katikati ni Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi.

Monday, February 10, 2014

BANDARI YA DAR ES SALAAM KUFANYAKAZI SAA 24

SERIKALI imesema tatizo la msongamano wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, utakuwa historia baada ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kuanza kufanyakazi saa 24.


Imesema utaratibu huo utaanza kutumika muda wowote kuanzia sasa na utaongeza tija na ufanisi kwa watumiaji wa bandari.

Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Dk. Shaaban Mwinjaka

Hatua ya kuanzisha utaratibu wa kufanyakazi kwa saa 24, imefikiwa na wadau wanaotumia bandari hiyo kwa ajili ya kuongeza huduma bora zinazotolewa na TPA.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, aliseama hayo jana mjini Dar es Salaam, kwenye hafla ya utiaji saini wa kufanyakazi kwa saa 24 kwa siku saba katika kipindi cha mwaka mmoja baina ya TPA na wadau wengine wa bandari.


Alisema utaratibu huo utapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa mizigo bandarini na kuongeza ufanisi wa utendajikazi.


“Tunataka kuwahakikishia wananchi kuwa utaratibu huu, utaboresha huduma zinazotolewa na TPA na utaondoa msongamano wa mizigo bandarini,” alisema.

Alisema serikali imeridhishwa na utaratibu huo na itahakikisha unafanikiwa ili kuondoa changamoto zilizokuepo bandarini hapo na kuleta ufanisi kwa watumiaji.
 

Dk. Mwinjaka katika kuhakikisha hilo linafanikiwa, tayari wametenga maeneo kwa ajili ya huduma za kibenki na kwamba nchi zingine wanazofanyanazokazi zitapatiwa maeneo ya ofisi.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPA, Madeni Kipande alisema utaratibu huo utaiwezesha bandari kufanyakazi kwa uhakika na ubora wa hali ya juu.

Friday, February 7, 2014

AIRTEL KUBORESHA MITAMBO YA HUDUMA ZA AIRTEL MONEY WIKENDI HII

· Mabadiliko yataleta ufanisi kwa huduma ya Airtel money
·Mabadiliko yatawezesha  wateja kufanya mambo mengi na kuongeza watumiaji wa huduma ya Airtel money
·  Mabadiliko yataongeza matumizi ya huduma ya Airtel money Tanzania

Dar es Salam, Tanzania 
Airtel Tanzania, kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma za kibunifu na zenye ubora nchini iko katika mchakato wa kuboresha mitambo ya huduma ya Airtel money na kuifanya kuwa ya kisasa zaidi.  Mabadiliko haya yatafanyika mwishoni mwa wiki hii  tarehe 7 hadi 9 februari 2014 ambapo baada ya maboresho hayo wateja wa Airtel Money watafurahia ufanisi bora wa mtambo wa Airtel money  wakati wowote watakapotaka kufanya malipo mbalimbali kwa kupitia huduma za kifedha  za simu za mkononi

 Maboresho hayo ya mitambo ya Airtel money wateja wataweza kufanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na  kuunganishwa na huduma mbalimbali na kuongeza ufanisi zaidi . Huduma hii itawawezesha wateja kununua muda wa maongezi, kutuma pesa, na kufanya malipo ya huduma mbalimbali, kutoa na kutuma pesa pamoja na kuongeza huduma mbalimbali wanazotakana kuzitumia kupitia Menu/orodha ya mpya ya huduma hiyo ya Airtel Money zikiwemo zile za kuunganishwa na huduma za kibenki

Akiongea kuhusu mabadiliko hayo ya mitambo, Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano Beatrice Singano Mallya (Pichani juu), alisema “kuboreshwa kwa mitambo yetu ya huduma za kifedha ya Airtel money  ni sehemu ya malengo ya Airtel ya kuwawezesha wateja wetu kufanya miamala ya pesa mahali popote wakati wowote kwa urahisi zaidi. Tunaamini maboresho haya yataleta urahisi zaidi kwa watumiaji wa huduma ya Airtel money nchini”

Bi Singano aliendelea kusema, “wakati wa kuboresha hatutegemei kuwa na matatizo yoyote wakati wa zoezi hilo la kuborehsha mitambo yetu na tunawaomba wateja wetu wawe wavumilivu kwa usumbufu utakaojitokeza wakati tutakapokuwa tunafanya zoezi hili kuanzia jumamosi saa 3 usiku hadi jumapili asubuhi . tunawahakikishia wateja wetu wa Airtel Money wote kuwa tunafanya mabadiliko yatakayoleta ufanisi zaidi kwa watumiaji wote,  mashirika binafsi, serikali, mabenki na wadau mbalimbali. Huduma yetu kwa wateja inapatikana masaaa 24 siku zote 7 za wiki ili kuweza kutoa huduma iwapo kutakuwa na matatizo yoyote. Pia tutaweza kuwasaidia wateja wetu watakaowasilisha baadhi ya matatizo kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii yaani Facebook and Twitter.”
Maboresho ya Airtel Money yenye lengo la kuendelea kutoa huduma Bora zaidi pia yanadhihirisha jitihada za Airtel kuendeleza ubunifu wa hali ya juu  kwa kuleta teknolojia mpya za kisasa zaidi katika sekta ya mawasiliano nchini Tanzania, Tumedhamiria kuwaletea wateja wetu huduma bora zaidi inayokwenda sambamba na mahitaji yao ya kila siku. Hii ndio sababu kubwa inayotufanya Airtel kuboresha mtambo wetu wa huduma hii ya Airtel Money kuwa wa kisasa zaidi.

Thursday, February 6, 2014

WASHINDI PROMOSHENI YA MIMI NI BINGWA WAPONGEZA AITEL,

Wakati Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel ikisubiria kuchezesha droo kubwa ya shilingi Milioni 50 kupitia promosheni ya Mimi ni Bingwa, baadhi ya washindi waliokwishapatikana wamejitokeza wakiisifia kampuni hiyo kwa kuratibu promosheni zenye kulenga maendeleo kwa watanzania walio wengi nchini.

Washindi hao wameainisha hayo muda mfupi baada ya kukabidhiwa pesa zao mapema wiki hii kwenye ofisi za makao makuu ya Airtel ziilizopo Morocco jijini Dar es salaam.

Washindi hao wamedai kuwa mara nyingi watu huwa hawaamini promosheni zinazoendeshwa na kampuni ya simu kama Airtel na hivyo kujikuta wakibaki nyuma kwa kuogopa kuthubutu.

“Mi binafsi sikuwahi kumuambia mke wangu kwamba nashiriki kwenye promosheni ya Mimi ni Bingwa sababu huwa akijua nashiriki ananikasirikia na kusema nina matumizi mabaya ya pesa, lakini leo nimeibuka mshindi wa shilingi milioni moja yeye akishuhudia na vilevile nimeshinda tiketi ya kwenda kushuhudia mechi ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford,” alisema mshindi huyo Bw. Msemwa Makuzi mkazi wa Dar es salaam.

Mshindi huyo aliendelea kwa kusema, kwa hali ya kawaida ilikuwa ni ngumu kuamini kwamba ameshinda shilingi milioni Moja na tiketi ya kwenda nchini Uingereza kushuhudia mechi ya Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford.

“Kweli mimi kama mtu mwingine yeyote wa kawaida iliniwia vigumu kuamini kwamba nimeibuka mshindi wa pesa hizo na tiketi. Na imenichukua muda kuamini mpaka sasa baada ya kukabidhiwa hizi milioni moja ndo naamini kweli mimi ni mshindi,” alimalizia Bw. Makuzi.

Aidha washindi wengine wamewaasa wananchi kote nchini kujitokeza kwa wingi katika promosheni hiyo kwani ina manufaa makubwa kwa maendeleo ya mtu binafsi na taifa zima.

“Kwa kweli mi nawaambia watanzania wenzangu wasidhani hivi vitu ni masihara, watu wanashinda kweli na maisha yao yanabadilika kupitia hizi pesa tunazopewa. Mimi hapa naiwinda hiyo milioni 50 kwani nina uhakika nikishinda nitakuwa nimesahau kabisa umasikini,” alisema Ramadhani Wefa ambaye ni mshindi wa milioni moja kutoka Kinondoni jijini Dar es salaam.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde alisema bado Airtel inatambua na itaendelea kutambua umuhimu wa wateja wake hivyo haina budi kuhakikisha inatoa huduma bora na zenye manufaa kwa wananchi wote kiujumla.
 “Airtel inaelewa fika kuwa wateja ndio kiini cha maendeleo ya kampuni hiyo na hivyo inajitahidi kuhakikisha inatoa huduma bora za kuwanufaisha wateja wake na kuleta maendeleo kwa taifa zima kiujumla,” alisema Jane.
Afisa Mahusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (wa pili kushoto) akiongelea umuhimu wa promosheni ya Mimi ni Bingwa muda mfupi baada ya kukabidhi shilingi milioni moja kwa baadhi ya washindi wa promosheni hiyo (waliopo pichani). Kushoto ni Bw. Ramdhani Wefa, Kulia ni Philemon Nathaniel Mgaya akifuatiwa na Bw. Msemwa Makuzi ambaye pia ni mshindi wa tiketi na wote wakiwa wanatokea Dar es salaam.