Friday, February 7, 2014

AIRTEL KUBORESHA MITAMBO YA HUDUMA ZA AIRTEL MONEY WIKENDI HII

· Mabadiliko yataleta ufanisi kwa huduma ya Airtel money
·Mabadiliko yatawezesha  wateja kufanya mambo mengi na kuongeza watumiaji wa huduma ya Airtel money
·  Mabadiliko yataongeza matumizi ya huduma ya Airtel money Tanzania

Dar es Salam, Tanzania 
Airtel Tanzania, kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma za kibunifu na zenye ubora nchini iko katika mchakato wa kuboresha mitambo ya huduma ya Airtel money na kuifanya kuwa ya kisasa zaidi.  Mabadiliko haya yatafanyika mwishoni mwa wiki hii  tarehe 7 hadi 9 februari 2014 ambapo baada ya maboresho hayo wateja wa Airtel Money watafurahia ufanisi bora wa mtambo wa Airtel money  wakati wowote watakapotaka kufanya malipo mbalimbali kwa kupitia huduma za kifedha  za simu za mkononi

 Maboresho hayo ya mitambo ya Airtel money wateja wataweza kufanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na  kuunganishwa na huduma mbalimbali na kuongeza ufanisi zaidi . Huduma hii itawawezesha wateja kununua muda wa maongezi, kutuma pesa, na kufanya malipo ya huduma mbalimbali, kutoa na kutuma pesa pamoja na kuongeza huduma mbalimbali wanazotakana kuzitumia kupitia Menu/orodha ya mpya ya huduma hiyo ya Airtel Money zikiwemo zile za kuunganishwa na huduma za kibenki

Akiongea kuhusu mabadiliko hayo ya mitambo, Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano Beatrice Singano Mallya (Pichani juu), alisema “kuboreshwa kwa mitambo yetu ya huduma za kifedha ya Airtel money  ni sehemu ya malengo ya Airtel ya kuwawezesha wateja wetu kufanya miamala ya pesa mahali popote wakati wowote kwa urahisi zaidi. Tunaamini maboresho haya yataleta urahisi zaidi kwa watumiaji wa huduma ya Airtel money nchini”

Bi Singano aliendelea kusema, “wakati wa kuboresha hatutegemei kuwa na matatizo yoyote wakati wa zoezi hilo la kuborehsha mitambo yetu na tunawaomba wateja wetu wawe wavumilivu kwa usumbufu utakaojitokeza wakati tutakapokuwa tunafanya zoezi hili kuanzia jumamosi saa 3 usiku hadi jumapili asubuhi . tunawahakikishia wateja wetu wa Airtel Money wote kuwa tunafanya mabadiliko yatakayoleta ufanisi zaidi kwa watumiaji wote,  mashirika binafsi, serikali, mabenki na wadau mbalimbali. Huduma yetu kwa wateja inapatikana masaaa 24 siku zote 7 za wiki ili kuweza kutoa huduma iwapo kutakuwa na matatizo yoyote. Pia tutaweza kuwasaidia wateja wetu watakaowasilisha baadhi ya matatizo kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii yaani Facebook and Twitter.”
Maboresho ya Airtel Money yenye lengo la kuendelea kutoa huduma Bora zaidi pia yanadhihirisha jitihada za Airtel kuendeleza ubunifu wa hali ya juu  kwa kuleta teknolojia mpya za kisasa zaidi katika sekta ya mawasiliano nchini Tanzania, Tumedhamiria kuwaletea wateja wetu huduma bora zaidi inayokwenda sambamba na mahitaji yao ya kila siku. Hii ndio sababu kubwa inayotufanya Airtel kuboresha mtambo wetu wa huduma hii ya Airtel Money kuwa wa kisasa zaidi.

0 comments:

Post a Comment