Wednesday, October 9, 2013

TPB YATANGAZA WASHINDI DROO YA MWISHO YA SHEREHEKEA MSIMU WA IDDI NA TPB WESTERN UNION

IMG_0159  
Meneja Mkuu Uendeshaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Kolimba Tawa (kulia) akimsoma mmoja wa washindi wa shindano la Sherehekea Msimu wa Iddi na TPB Western Union leo jijini Dar es Salaam.
IMG_0134  
Meneja Mkuu Uendeshaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Kolimba Tawa (wa pili kulia) akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa shindano la Sherehekea Msimu wa Iddi na TPB Western Union leo jijini Dar es Salaam akimjulisha ushindi wake.
IMG_0101  
Mmoja wa vijana maalumu akikabidhi moja ya kuponi baada ya kuitoa kwenye boksi ili kumpata mmoja wa washindi wa shindano la Sherehekea Msimu wa Iddi na TPB Western Union.
IMG_0092  
Mmoja wa vijana maalumu wakichanganya kuponi kwenye boksi kabla ya kuchagua moja wapo ili kumpata mshindi wa shindano la Sherehekea Msimu wa Iddi na TPB Western Union.
Na Joachim Mushi, Dar
  BENKI ya Posta Tanzania (TPB) hatimaye leo imewataja washindi wa droo ya mwisho wa Shindano la Sherehekea Msimu wa Iddi na TPB Western Union lililokuwa likiendeshwa na benki hiyo. Akizungumza katika hafla fupi na wanahabari jijini Dar es Salaam ya kuwataja washindi hao nane, Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa alisema zoezi hilo ni mwendelezo wa benki hiyo katika kurejesha sehemu ya mapato ya benki kwa wateja wake. Alisema washindi hao nane kwa jumla wamejishindia shilingi milioni 1.5. Akifafanua zaidi alisema mshindi wa kwanza ambaye ni Elias Mwalamala kutoka Dar es Salaam amejishindia sh. 500,000/-, na mshindi wa pili, Nathan Gawangi kutoka Kigoma akijipatia kitita cha sh. 300,000/-, huku mshindi wa tatu Bruno Hindu (Dar es Salaam) akifanikiwa kuibuka na sh. 200,000/-. Alisema washindi wengine watano ambao nao benki hiyo itawazawadia sh. 100,000/- kila mmoja ni pamoja na Miss Farida kutoka Zanzibar, Alfa Mwakalinga wa Dodoma, Mariam Mtungo, Ramadhan Mapuya kutoka pamoja na Fadhili Daud Mbaga wote kutoka Dar es Salaam. Aidha Tawa aliongeza kuwa washindi wote watapigiwa simu na uongozi wa TPB na kuelekezwa namna ya kupata zawadi zao waliojishindia wakiwa ni miongoni mwa wateja waliotuma na kupokea fedha kupitia huduma ya Western Union. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

0 comments:

Post a Comment