SERIKALI imesema tatizo la msongamano wa
mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, utakuwa historia baada ya
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kuanza kufanyakazi saa 24.
Imesema utaratibu huo utaanza kutumika muda wowote kuanzia sasa na utaongeza tija na ufanisi kwa watumiaji wa bandari.
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Dk. Shaaban Mwinjaka |
Hatua ya kuanzisha utaratibu wa kufanyakazi kwa saa 24, imefikiwa na wadau wanaotumia bandari hiyo kwa ajili ya kuongeza huduma bora zinazotolewa na TPA.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, aliseama hayo jana mjini Dar es Salaam, kwenye hafla ya utiaji saini wa kufanyakazi kwa saa 24 kwa siku saba katika kipindi cha mwaka mmoja baina ya TPA na wadau wengine wa bandari.
Alisema utaratibu huo utapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa mizigo bandarini na kuongeza ufanisi wa utendajikazi.
“Tunataka kuwahakikishia wananchi kuwa utaratibu huu, utaboresha huduma zinazotolewa na TPA na utaondoa msongamano wa mizigo bandarini,” alisema.
Alisema serikali imeridhishwa na utaratibu huo na itahakikisha unafanikiwa ili kuondoa changamoto zilizokuepo bandarini hapo na kuleta ufanisi kwa watumiaji.
Dk. Mwinjaka katika kuhakikisha hilo linafanikiwa, tayari wametenga maeneo kwa ajili ya huduma za kibenki na kwamba nchi zingine wanazofanyanazokazi zitapatiwa maeneo ya ofisi.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPA, Madeni Kipande alisema utaratibu huo utaiwezesha bandari kufanyakazi kwa uhakika na ubora wa hali ya juu.
hili litapandisha uchumi wetu
ReplyDelete