This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Friday, July 27, 2012

RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINMGI UJENZI HANGA LA PRECISION AIR DAR

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kuzindua rasmi  hanga la Precision Air lililopo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Precision Air Bwana Michael Shirima.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi hanga la Precisionair katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa  Julius Nyerere leo asubuhi.Kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt.Harrison Mwakyembe na kulia ni mwanzilishi na Mwenyekiti wa Precision air Bwana Michael Shirima.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia moja ya ndege za shirika la ndege la Precision ikifanyiwa matengenezo katika hanga jipya la shirika hilo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
 Mwenyekiti wa Precisionair Bwana Michael Shirima akimwongoza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kutembela hanga jipya la shirika hilo la ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 Mwenyekiti wa Precisionair Bwana Michael Shirima akimwongoza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kutembela hanga jipya la shirika hilo la ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 Mwenyekiti wa Precisionair Bwana Michael Shirima akimwongoza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kutembela hanga jipya la shirika hilo la ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na mwenyekiti wa Precisionair Bwana Michael Shirima wakati wa hafla ya uzinduzi wa Hanga la shirika hilo la ndege lililojengwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu  Julius Nyerere(picha na Freddy Maro) 

Wednesday, July 18, 2012

VIDACOM NA NOKIA WASHIRIKIANA KUPUNGUZA GHARAMNA ZA SIMU

*       Ushirikiano huo ni katika kuwanufaisha vijana.
*       Ofa ya simu ni Nokia Asha 200 na Niokia Asha 302
*       Wateja kupata ya intanet bure kwa miezi sita, huduma ya facebook, twitter na Wikipedia kuendelea kuwa bure.                                                                                                                                                 DAR ES SALAAM, TANZANIA
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imeingia katika ubia na kampuni ya Nokia katika kutoa ofa ya aina mpya ya simu za Nokia kwa Watanzania.

Aina ya simu ambazo zimeingizwa katika ofa hiyo mpya ni simu aina ya Nokia Asha 200 na Nokia Asha 203 ambazo ni katika mpango maalum wa Vodacom wa kupunguza gharama za huduma za simu kwa vijana.

 Kupitia simu hizo, wateja wataweza kupata huduma nafuu kwa simu ya Nokia Asha 200 inayouzwa kwa shilingi 149,999 na watapata muda wa bure wa maongezi na MB 125. Kwa simu ya Nokia Asha 302 inayouzwa kwa shilingi 219,000 wateja watapata MB 500 kwa miezi sita mfululizo baada ya kuweka muda wa maongezi wa Shilingi 1000, 2000, au 5000 huku huduma ya facebook, twitter na Wikipedia zikiendelea kuwa bure.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ofa hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Vifaa wa kampuni ya Vodacom Tanzania Bw. Mngopelinye Kiwanga, amesema kuwa ofa hiyo inalenga kuongeza soko kwa kampuni hiyo na kukuza utoaji wa huduma na  uuzaji wa bidhaa, na kuongeza kuwa vijana, ambao wanachukua idadi kubwa ya watu katika taifa, ni vyema wakapata huduma nafuu za mawasiliano ili kuchangia katika ukuaji wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

"Tunaamini kwa mpango huu, tutawafikia wateja wengi zaidi iwezekanavyo," alisema Kiwanga, na kuongezea kuwa kutakuwa na maboresho mbalimbali  ya mtandao na ubora wa bidhaa, suala litakalo wawezesha wateja kufikiwa na huduma na kutanabaisha kuwa zipo ofa nyingi na bidhaa ambazo kampuni hiyo inatarajia kutoa kwa wateja wake ndani ya Mwaka huu.

" Napenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa tutaendelea kuboresha na kuleta huduma nzuri na bora kwa ajili yao ili kukidhi mahitaji yao ya kila siku na kuwa na mahusiano mazuri na wateja wetu," alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Nokia Tanzania Samson Majwala, amesema kuwa simu hizo zina sifa nzuri na ni rahisi kuzitumia, suala ambalo litawavutia watu wengi kununua na kuzitumia kwa urahisi.

"Simu hizi ni nzuri na rahisi kutumia. Nina imani kuwa wateja watafurahia na  kuzitumia," alisema Majwala. PICHANI,Meneja Mkuu wa Nokia Tanzania Samson Mwajwala,akionesha aina ya simu ya Nokia Asha 200 inayouzwa kwa shilingi 149,999 pamoja na  muda wa bure wa maongezi na MB 125.Simu ingine ya Nokia Asha 302 inauzwa kwa shilingi 219,000 wateja watapata MB 500 kwa miezi sita mfululizo baada ya kuweka muda wa maongezi wa Shilingi 1000, 2000, au 5000 huku huduma ya facebook, twitter na Wikipedia zikiendelea kuwa bure,katikati Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa Vodacom Tanzania Bw. Mngopelinye Kiwanga na Meneja bidhaa wa Vodacom Elihuruma Ngowi.

AIRTEL INTRODUCES FIRST MOBILE COMMERCE SERVICE IN BURKINA FASO

•   A first in Burkina Faso, this facility enables consumers top up air time on their phones directly
•   Retailers to benefit through additional revenue, creation of employment and new business opportunities
•   Significant benefits for Burkina Faso’s informal ecosystem
 OUAGADOUGOU, Burkina-Faso, July 18, 2012/ -- Airtel Burkina Faso (http://www.airtel.com), the largest mobile company in the country, has launched its mobile money platform named Airtel Money, or m-ligdi, in partnership with Ecobank. The platform allows consumers to top up their phones with air time, send and receive money, pay their critical utility bills, access their bank accounts.
     The press conference for the launch took place in Ouagadougou and was attended by  the Minister of Transport, Post and the Digital Economy, the Minister of Economy and Finance, the national Director of the Central Bank of West Africa States, the CEO of the Regulatory Authority and the managing directors of Airtel Burkina Faso and Ecobank.
    In many developing regions, including Africa, the availability of formal financial services is limited to certain geographic and income ranges, often leaving the majority of the population to rely on unreliable and costly informal channels for their financial transactions. Against this backdrop, the total value of mobile money transfers in Africa is estimated to exceed US$200 billion in 2015 due to users’ growing trust in the system and the growing range of services provided. Key market players, banks and mobile operators in particular, are keen to address this opportunity.
     Commenting on the launch, John Ndego, Airtel Managing Director said: “Today is a very important day for us as we introduce Airtel Money in Burkina Faso to address this much needed gap by providing access to banking services, initially through money transfers and purchase of goods and services through electronic payments.”
     He continued “On a day to day basis with Airtel Money, you no longer have to carry cash. All you need is your mobile telephone. This service allows customers to send money to loved ones, pay essential utility bills such as electricity or water, settle grocery bills in the supermarket and even top up your phone with airtime.”
     According to Cheikh Travaly, Director of Ecobank, "Everything is done to fully support the efforts of Airtel SA Burkina Faso in order to improve the lives of our people with this new electronic payment service. Ecobank will support Airtel to ensure that the product being launched is efficient and secure. We encourage everyone to take advantage of this great service. "
      "I would therefore like to congratulate Airtel for launching this service and I am sure it will be highly appreciated by many in Burkina Faso. The service will extend the financial inclusion program launched by Ecobank in Burkina Faso and will have a tangible positive impact on the community, "he added.
      Airtel Money, strengthen its commitment to provide affordable and innovative solutions to all. The platform, allows consumers and communities to take maximum advantage of the mobile commerce reality sweeping through the industry by enabling them to conduct a range of financial transactions quickly and easily.
     Aside from the direct transfer of funds from one user to another, Airtel Money also simplifies the lives of its customers by allowing them to conduct a range of other financial transactions using their handsets such as bill payments, top ups and mobile banking.
      The transactions will be very simple and also completely secure. All a customer needs is a mobile phone and a personal password every time they want to carry out a transaction. To benefit from this service, a simple registration process is required. The customer should be an Airtel Customer, have a valid ID document and fill out a registration form.
      Mr. Ndego reiterated Airtel’s commitment to ensure that Airtel Money will be available in all the regions where the network is available. He also encouraged customers to take advantage of this service.
      Distributed by the African Press Organization on behalf of Bharti Airtel Limited.

SOURCE 
Bharti Airtel Limited

UNSUBSCRIBE

Friday, July 13, 2012

VODACOM KUWATUZA WAANDISHI MAHIRI WA MITANDAO YA JAMII NA TOVUTI NCHINI

·         Waandishi wa mitandao ya kijamii na tovuti kupewa tuzo 
kutokana na jitihada na mafanikio yao.
·         Tuzo hizo kuitwa “ Tuzo za umahiri wa digitali za Vodacom”

Dar es Salaam, 11 julai, 2012
 Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, itatoa tuzo kwa waandishi bora kumi mahiri katika mitandao ya kijamii kutokana na umahiri wao.
Tuzo hizo ambazo zimepewa jina la “Tuzo za Umahiri wa Digitali za Vodacom”, zitatolewa kwa washindi kumi kutokana na jitihada zao na mafanikio yao ikiwa ni kwa mara ya Kwanza kufanywa na kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema kuwa Waandishi wa mitandao ya kijamii wanao mchango mkubwa katika kutoa taarifa mbalimbali ndani ya jamii, na mchango huu unatakiwa kuthaminiwa.
Wapo waandishi wengi katika mitandao ya kijamii na wanaandika masuala mbalimbali kuhusu biashara au hata yale yanayogusa jamii moja kwa moja, Ni kwa sababu hii ndio maana tunatambua na kuwapatia tuzo hizi kutokana na mabadiliko waliochangia katika utoaji wa taarifa” Alisema Meza.
Baadhi ya sifa ambazo zitapewa kipaumbele katika tuzo hizi, pamoja na mambo mengine, ni ubunifu na utoaji wa taarifa za kijamii,  Kuzingatia ueledi wa uandishi na uhuru wa vyombo vya habari, mahusiano na wasomaji katika utoaji wa taarifa, umahiri wa picha na ushirikishwaji wa vyombo vingingine.
Waandishi wa mitandao ya kijamii wata shindanishwa kadri inavyowezekana ili kuwawezesha kuongeza ueledi na umahiri katika kazi zao.
Kampuni ya Vodacom Tanzania pia itaanzisha  mfuko wa fedha wa maendeleo ya digitali, Kwa mujibu wa Meza fedha hizi zitatumika katika kuendeleza umahiri na kuboresha kazi katika mitandao ya kijamii na tovuti.“Huu ni mchango kutoka Mfuko wa M-pesa ambapo waombaji wataweza kuzitumia katika udhamini na kuendeleza shughuli zao”, Alisema Meza na kuongeza kuwa, “ Tunathamini mchango wa kila mtu, na tunahitaji waandishi wa mitandao ya kijamii wote waendelee kufanya kazi zao nasi tutaendelea kuthamini na kutambua mchango wao na kuwapa tuzo.”

Thursday, July 12, 2012

Vodacom kuwapa wateja wake mara TANO zaidi kwa kila kifurushi cha Intaneti


·        Wateja kuendelea kuperuzi Wikipedia, Facebook na Twitter bure
·        Ofa mpya kuwapa wateja wanaotumia intaneti huduma bora zaidi

Dar es Salaam July 12, 2012 
Wateja wa Kampuni ya Vodacom wana fursa nyengine murwa ya kufurahia mawasiliano kupitia njia ya intaneti ambapo sasa watapokea mara tano zaidi ya kila kifurushi cha data wanachonunua kupitia Vodacom kwa gharama nafuu.

Ofa hiyo inanuia kupanua wigo ya ofa zinazotololewa sokoni wakati huu kupitia kampeni maarufu ya Wajanja.

Ofa hii inaenda sambamba na ofa inayoendelea kwa wateja wa malipo kabla ambayo inawawezesha kuperuzi Wikipedia, Facebook na Twitter bure kila siku, ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha wateja wanafaidi zaidi na kubakia wakiwa wameunganishwa katika mitandao ya kijamii.

“Kila mmoja kuanzia wanafunzi, wafanyakazi, wafanyabishara na wengineo wana nafasi yake kutumia huduma za Intaneti kupata taarifa za masuala mbalimbali. Hivyo ni muhimu kuwapatia watu BURE huduma za kuperuzi kama vile Wikipedia hususan wanafunzi ili kuwawezesha kupata kwa haraka taarifa muhimu wanazozihitaji katika masomo,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza

“Kwa kiasi kidogo cha Sh 250 kwa siku mteja wetu anapata 25MB ikiwa ni mara tano zaidi ya aliyokuwa akipata hapo awali ikimaanisha kwamba anaweza kuperuzi mtandao wa google na mengineyo kwa kasi zaidi na kuunganishwa na ndugu na marafiki,” ameongeza kusema Bw. Meza akidokeza kuwa kampeni ya Wajanja ambayo imehusisha pia matamasha ya burudani ya muziki sehemu mbalimbali ya nchi imekuwa na mafanikio makubwa na itazidi kubuni na kutoa ofa zaidi kumwezesha kila mmoja kutumia gharama nafuu katika mawasiliano. 

Vifurushi vingine vinavyopatikana katika ofa hii ya pata tano zaidi ni 50MB kwa Sh 450 kwa siku, 150MB kwa Sh 2,500 kwa siku saba na 100MB  kwa Sh 2000 kwa matumizi ya siku thelathini.

Kujiunga na kununua vifurushi vya Intaneti za Vodacom ni rahisi. Mteja anahitajika kupiga *149*01# na kasha kuchagua aina ya huduma na kifurushi anachokihitaji.

Wednesday, July 4, 2012

MAONYESHO YA SABASABA LEO

 Watu wakiingia kwenye vianja vya Sabasaba, kwenye maonyesho yanayoendelea kwenye viwanja hivyo
Moja ya bidhaa zinazopendwa ni magodoro
 Baadhi ya wafanyabiashara wanalazimika kupumzika kama hivi, kwenye viwanja hivyo ya Manonyesho ya Sabasaba
  Wafanyabiashara Steven na Ken kutoka Canton, China wakiwa kwenye banda lao
 Steven na Ken wa  Canton, China wakiwa kwenye banda lao
 Watoto wakipata fursa ya kucheza kwenye viwanja vya Sabasaba
 Kwenye banda la vinywaji baridi la Cocacola nako mambo yakawa moto moto kama hivi
 Hii ni ATM ya benki ya NMB ndani ya Uwanja wa Saba saba
Shamba la mfano la Jeshi la Magereza ndani ya Viwanja vya Sabasaba

Sunday, July 1, 2012

AFRICAN TRADE INSURANCE AGENCY ' YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA DAR, YAIPA TUZO KAMPUNI YA BAKHRESA

 Mmoja wa wakurugenzi wa African Trade Insurance (ati) Japhet Vincent akizungumza wakati wa Coctail ya kampuni hoyo na wafanyabiashara iliyofanyika kwenye hoteli ya 'Kilimanjaro' Dar es Salaam. Pamoja na kujitambulisha kwa wafanyabiashara hao ati ilitoa tuzo kwa kampuni ya Said Salim Bakhresa & Co ya jijini Dar es Salaam, kwa kuwa mmoja wa wadau wakubwa wa kampuni hiyo kubwa ya Bima ya Wafanyabiashara binafsi na nchi.
 Mkurugenzi wa  Kampuni hiyo ya Bima Kanda ya Afrika,  Basil Saprapasen akizungumza wakati wa hafla hiyo.
 Uongozi wa kampuni hiyo ukiwa na tuzo tayari kumkabidhi mwakilishi wa kampuni ya Bakhresa
Basil na Vincet wakimkabidhi tuzo Meneja Mkuu (Biashara) wa Kampuni ya Saidi Salim Bakhresa & Co Ltd, Saibal Sarbadhikari, wakati wa Coctail hiyo
 Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation (tpsf) ambao ni wa dau wa ati, Godfrey Simbeye akizungumza bada ya utoaji wa tuzo hiyo.
 Kikundi cha ngoma za 'mabuti' kikitumbuiza wakati wa hafla hiyo
 Badhi ya walioalikwa
  Baadhi ya waalioalikwa na viongozi wa ati
Mwanamuziki mahiri wa siku nyingi hapa nchini Zahir Ali 'Zoro' akiwa na mtoto wake, Baba Zoro wakati walipokuwa akitumbuiza na bendi yao ya B Band kwenye haflahiyo.