Saturday, February 16, 2013

NSSF YAPIGA HODI ZANZIBAR

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akipeana mkono na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Juma Kintu.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulembe wakati ujumbe kutoka shirika hilo ulipofika ofisini kwake kuandikisha viongozi wa Serikali katika Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF mjini Zanzibar leo.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akijaza fomu ya uanachama wa Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na ujumbe kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuhusu Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiweka saini ya dole gumba.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Ofisini Kwake Vuga mjini Zanzibar baada ya kujiunga na NSSF. Kushoto ni Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Dodoma, Mariam Ahmed, Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu na Ofisa Uendeshaji NSSF, Ally Mkulemba. 
 Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akimkaribisha ofisini kwake Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed alipofika kwa ajili ya Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo.
 Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akifafanua jambo kuhusu Mpango Maalum wa Hiari wa kuchangia Mafao ya NSSF kwa viongozi wa Serikali mjini Zanzibar leo. Kulia ni Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud.
  Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akimpa maelekezo ya kujaza fomu ya uanachama wa NSSF, Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud.
 Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akiweka saini ya dole gumba.
 Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akimpa maelekezo ya kujaza fomu ya uanachama wa NSSF, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Said Shaaban Said.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mariam Ahmed akimpa maelekezo ya kujaza fomu ya uanachama wa NSSF, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Said Shaaban Said.


Na Mauwa Mohammed, Zanzibar

MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  amesema Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Tanzania (NSSF) utafanya  utaratibu wa kuishawishi mifuko mengine ya Jamii kuanzisha  miradi ya Jamii ili kuongeza pato la wanachama pamoja na Maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Kauli hio alitoa  wakati  akijaza fomu maalum ya kuomba kujikunga kuwa mwanachama rasmi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii { NSSF }  hafla iliofanika  Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar

Alisema mfuko huo umeonyesha mwanga na matumaini makubwa kwa wanachama wake hasa kutokana na miradi mingi iliyoianzisha ambayo kwa Asilimia kubwa inalenga kuwanufaisha wanachama wake hasa wale wenye kipato cha chini.

Balozi Iddi alisema NSSF ni chombo cha wananchi kwa vile kinajihusisha moja kwa moja na hatma ya washirika wake ambao wengi wao ni wafanyakazi wenye kipato cha chini.

Aliuahidi Uongozi wa Mfuko huo wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwamba amehamasika ya mfumo wa mfuko huo na kupelekea moja kwa moja kuamua kujiunga ambapo ameahidi kuchangia kila baada ya kipindi cha miezi mitatu.

Mapema Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii { NSSF } Mkoa wa Dodoma ambao ndio uliopewa jukumu la kuhudumia Viongozi wa ngazi ya Juu Bibi Maryma Ahmed alisema  zaidi ya Wabunge 165 wamekubali kujiunga kwa hiari kuwa wanachama wa Mfuko huo.

Bibi Maryam alimueleza Balozi Seif kwamba wabunge hao hupatiwa mafao yao mara wamalizapo utumishi wao wa Bunge sambamba na huduma za matibabu wakati wa kipindi chote cha kazi zao.

Hata hivyo Meneja huyo wa NSSF Kanda ya Dodoma alieleza kuwa wapo Wabunge wastaafu waliomaliza wadhifa wao lakini bado wanaendelea kuchangia mfuko huo kwa vile bado wana fursa iliyo wazi ya kufanya hivyo.

Nae waziri  katika afisi ya Makamom wa pili wa rais Mohamme Aboud Mohammed amesema wananchi wa Zanzibar bado hawajapata mwamko mzuri wa kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF.

Alisema wananchi wengi watakuwa tayari kujiunga na mfuko huo endapo wataelimishwa juu ya faida watakozipata kwa kujiunga na mfuko huo.

Alisema ni vyema wakulima wa karafuu , wavuvi na wajasiri amali wadogo wadogo kuelimishwa ili wapate kujiuna na mfumo huo kwa lengo la kuwasaidia.

 Meneja   wa NSSF Mariyam Mohammed alisema  wajasiri amali wadogo wadogo na sekta zisizo rami watafaidika  endapo watajiunga na mfuko huo wa hiari  ambao utasaidia   maisha yao ya baadae.

Alisema wafanyikazi  wa sekta zisizo rasmi kabla  haujanzishwa mfuko huo wa hiri walikuwa hawachukuliwi na sekta nyengine yeyote isipokuwa yule aliyeajiriwa katika sekta binafsi tu.

Hivyo mfuko huo  wanachama wake wataweza kupata mafao yao saba yakiwemo ya kumia kazini,msaada wa uzazi kwa mama waja wazito,msaada wa mazishi , pamoja na mfuko wa afya.

“Kina mama waja wazito watafaidika na  mafao ya mfuko wa hiari endapo  watajiunga na mfuko huo”alisema Bi Maryam .

Mafao mengine yatakuwa ni baada ya muda miaka mitatu   kuchangia  mfuko huo  ni mafao ya pensheni ya ulemavu ,  pensheni  urithi na  pensheni ya uzee .

Alisema wanachama wengi wasio rasmi wanapata shida ya matibabu kwa vile hawana kiasi rasmi cha fedha ambazo wataweza kujitibia hivyo kujiuna na mfumo huo wa hiyari watapata matibabu ya bure endapo watapata matatizo ya  kiafya pamoja na familia zao.

Balozi Seif amesajiliwa kuwa mwanachama wa Mfuko huo wa Taifa Hifadhi ya Jamii baada ya kukamilisha taratibu zote za kujaza fomu ya usajili mbele ya Timu ya Maafisa wa mfuko huo ikiwemo pia kupigwa picha kwa ajili ya kupatiwa kitambulisho rasmi cha uwanachama kamili wa mfuko huo.

0 comments:

Post a Comment