Mhe: Mgeni Rasmi Waziri wa Uwezeshaji na uwekezaji Mama Marry Nagu.
Awali ya yote tunachukua fursa hii Kukushukuru kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika shughuli yetu hii muhimu inayowahusu wajasilia mali wa Vicoba wanaoratibiwa na PFT katika Manispaa ya Temeke na tunakukaribisha karibu sana Temeke na ujisikie upo Nyumbani
.
1. UTANGULIZI.
Poverty Fighting Tanzania (PFT) ni Taasisi isiyo ya kiserikali lililosajiriwa chini ya sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) sheria namba 24 kifungu kidogo cha 12 sheria ya mwaka 2002 kwa namba ya usajiri 00NGO/00004071.
Ofisi za PFT zipo Mtaa wa Kitunda Tandika Wilaya ya Temeke,Mkoa wa Dar-es-salaam.
2. Muundo wa PFT:
Mhe: Mgeni Rasmi: PFT inaongozwa na Mkutano mkuu hiki ndio chombo cha juu katika kufanya maamuzi yanayohusina sera,na taratibu za PFT, ikifuatiwa na Bodi ya wakurugenzi na Menejimenti ambayo inasimamia kazi za siku hadi siku inayoongozwa na mkurugenzi Mtendaji.
3. Lengo la PFT:
Mh: Mgeni Rasmi:
Lengo la PFT: Ni kuunganisha Nguvu kazi katika kupambana na Umasikini Tanzania.
Dira ya PFT: Kujenga jamii ambayo itakuwa huru kutokana na umasikini na maradhi .
Dhamira ya PFT: Kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya jamii kupitia kuanzisha vikundi vilivyoandaliwa na kuwezeshwa kwa ustadi na mitaji ya kutosha.
Mhe: Mgeni rasmi: Kutokana na malengo hayo PFT inatekeleza shughuli zifuatazo:
· Kuhamasisha na kuunda vikundi vya Vicoba katika ngazi chini yaani Grassroots level
· Kuwajengea uwezo wanachama wa PFT katika maeneo makuu matatu:
i. Mfumo wa Vicoba namna unavyofanya kazi
ii. Stadi za uongozi wa vikundi na ujasilia mali
iii. Kuwaunganisha wanachama wa Vicoba wa PFT na wadau wengine wa maendeleo kwa lengo la kujenga ubia na kubadilishana uzoefu,taarifa, maarifa na kupanua masoko yao.
4. Walengwa wa mradi:
Mhe: Mgeni Rasmi:
Katika kutekeleza program ya kupunguza umasikini ,walengwa wa mradi huu ni familia zenye kipato cha chini ,jamii iliyoko pembezoni mwa huduma za kifedha na makundi maalumu.
5. Mafanikio ya mradi huu:
Mhe: Mgeni rasmi: Hadi kufikia sasa PFT imefanikiwa kuunda jumla ya Vikundi 130 venye wanachama 2,228 wanawake wakiwa 1,956 sawa na asilimia 87.8 na wanaume wakiwa 272 sawa na asilimia 12.2 wanachama hao wamewekeza jumla ya Tshs: 833,967,140 kupitia mpango wa ununuzi wa hisa za kila wiki na kuchangia mfuko wao wa jamii, fedha zote hizo zinamilikiwa na wanakikundi wenyewe kupitia akaunti zao 105 zilizofunguliwa Amana Benki zinazotumika kuifadhi fedha za mizunguko yao na marejesho ya mikopo yao wanayokopeshana.
Jumla ya mikopo 1,240 yenye thamani ya Tshs: 584,729,000 imetolewa na wana vikundi wenyewe kupitia mifuko yao ya hisa.
Mhe: Mgeni Rasmi Jumla ya Tshs: 75,779,900 zimegawiwa kwa wanachama hao ikiwa faida itokanayo na mikopo wanayokopeshana kwa kipindi cha miaka 3 sasa.
Mhe: Mgeni Rasmi pia tumefanikiwa kuwaunganisha wanachama wa PFT na Taasisi ya kifedha yaani Amana Benki ambayo imekubali kuwakopesha wanachama hao kupitia PFT jumla ya Tshs: 300,000,000 kwa kuthaminisha bidhaa wanazohitaji wanachama wa PFT ili waweze kukuza shughuli zao za kiuchumi, miongoni mwa mikopo hiyo ndiyo hii ambayo leo utakabidhi gari aina ya Suzuki carry 6 ,Bajaj 10, Pikipiki aina ya Boxer 19, toyo la kubebea mizigo 1, vifaa vya selemala vinavyotumia umeme, mbao,vifaa vya statiories na vifaa vya shooting Camera kwa vikundi 19 vinavyoratibiwa na PFT vyote vikiwa na thamani ya Tshs: 192,321,000/=
6. Changamoto
Mhe Mgeni Rasmi :
Pamoja na mafanikio yote hayo bado PFT inakabiliwa na changamoto nyingi katika kutimiza malengo yake baadha ya changamoto hizo ni:
i. Ugumu wa upatikanaji wa mikopo ya masharti nafuu, kwani hata huu mkopo tuliyopata amana tumechukua muda mrefu zaidi ya 5 na Dhamana kubwa iliyowekwa ndio tumefanikiwa kupata mkopo huo kwaiyo hiyo changamoto inayowasumbua wajasilia mali wengi wadogo Tanzania.
ii. Upungufu wa fursa za kupata elimu ya ujasilia mali zaidi kwa wanachama wetu na kujenga ubia na wadau wengine wa ndani na je ya nchi kupitia wizara ya uwezeshaji na uwekezaji .
7. Hitimisho:
Mhe: Mgeni Rasmi :
Mwisho tunaludia tena kukushukuru wewe binafsi na msafara wako mliongozana nao kuja katika shughuli hii muhimu kwa wajasilia mali wa Temeke, PFT ina imani kubwa na wewe.
Mhe: Mgeni Rasmi : Sisi tunakujua kuwa una moyo na upendo kwa PFT na hiyo imedhirika tena kwa mara ya pili leo,kwani mara ya kwanza Tulikutana ofisini kwako Dodoma mwezi February 2013 ulikuwa na majukumu mengi na msarafa wetu ulikuwa wa ghafla sana lakini ulitupokea na kutusaidia kwa kutuunganisha na Viongozi wa Baraza la uwezeshaji la Taifa ahsante Mhe: Waziri.
Mhe: Mgeni Rasmi: kupitia kwako Menejimenti , Bodi ya Wakurugenzi na wanachama wote wa PFT tunampongeza sana mwenyekiti wetu wa bodi Mhe; Abbas Mtemvu ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa usimamizi wake makini wa PFT hadi kufikia mafanikio haya.
Imani yetu ni kwamba utaendelea kushirikiana nasi na kutusaidia mara kwa mara kwa kadri ya uwezo wako ili wajasilia mali hawa wa Temeke waweze kufaidika na fursa zinazotokea katika wizara yako ambazo zinawalenga wao.
Tunakutakia kila heri na mafanikio katika utendaji wako wa majukumu ya kitaifa,Sisi PFT tutaendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha tunatekeleza mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini wa kipato Tanzania (MKUKUTA II)
Karibu tena Temeke wewe na msarafa wako
Naomba kuwasilisha:
VICOBA SILAHA DHIDI YA UMASIKINI
NI MARUFUKU KUKATA TAMAA
Friday, January 24, 2014
TAARIFA FUPI KWA MHE: WAZIRI WA UWEZESHAJI NA UWEKEZAJI MAMA MARY NAGU KUHUSU POVERTY FIGHTING TANZANIA (PFT) TAREHE 24/01/2014 PTA SABA SABA
4:33 AM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment