This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Sunday, December 23, 2012

KAMPUNI ZA NDEGE ZINAZOTOA HUDUMA KUPITIA M-PESA ZAONGEZEKA


DAR ES SALAAM, Tanzania
Idadi ya Kampuni na Mashirika ya ndege nchini ambayo yameingia kwenye mkataba na Vodacom katika kuwawezesha wateja wake kulipia tiketi za usafiri huo kupitia M-Pesa imeongezeka.

Hadi kufikia sasa Kampuni zilizoingizwa moja kwa moja kwenye mfumo wa huduma hiyo ni pamoja na Shirika la Ndege la Precision, Coastal Travels, Auric Air na Skylink Tanzania. Huku Kampuni nyingine zikipatikana kwenye orodha kwa kuingiza namba ya biashara ya kampuni husika.

Ili kufanya malipo mteja atatakiwa kupiga namba *150*00# na kuchagua malipo ya bili kupitia orodha ya M-pesa na kuingiza namba ya biashara ya Shirika au Kampuni husika ikifuatiwa na namba ya malipo na kiasi cha fedha itakayolipwa.

Mkuu wa Kitengo cha Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa, amesema kuwa njia hiyo ni ya haraka, rahisi na itaokoa muda kwa wateja, hususan katika msimu huu wa sikukuu za Krismass na Mwaka mpya, ambapo wateja wengi hupendelea kusafiri.

Amesema Vodacom inaona fahari kuingia katika ushirikiano huu na wabia wake, kwani kwa kufanya hivyo huduma husika itasaidia kuondoa foleni na misongamano ambayo ni dhahiri inapoteza muda wakati wa ukataji tiketi.

Aidha ameeleza faida za huduma hiyo kuwa ni pamoja na kukata tiketi ukiwa popote, pia hakuna sababu ya kutembea na fedha taslimu, hatua inayomhakikishia usalama mteja, na pia mteja akikata tiketi papo hapo atapata salio la bure la muda wa maongezi wa shilingi 1000.

Aidha, Twissa anaeleza kuwa ushirikiano huo utatoa njia mbadala katika malipo ya tiketi, na kusisitiza kuwa huduma ya M- pesa ni salama, haraka na ya uhakika, kwa kuwa imeleta mapinduzi katika huduma mbalimbali za kifedha tangu kuanzishwa kwake miaka minne iliyopita.

"Tunaamini kuwa tutaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wetu. Tunajivunia ushirikiano huu na tunatarajia utakuwa na mafanikio makubwa katika kukidhi mahitaji ya huduma kwa wateja wetu," anasema Twissa.

Huduma ya M-Pesa ya Vodacom Tanzania ina mawakala zaidi ya elfu 20,000 nchini kote, na ni pekee ambayo inaongoza, kwa usalama na ubora katika kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha kwa Watanzania walio wengi.

Friday, December 21, 2012

NOKIA PROMOSHENI


Mkazi wa Buza nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Eusedia Donald, (katikati) akipokea zawadi ya simu aina ya Nokia 302 kwenye duka la Vodacom lililopo eneo la Mlimani City Dar es Salaam jana, kutoka kwa Meneja Mauzo wa duka hilo Salim Salmin (Kulia) kufuatia promotion ya shinda na Nokia inayoendelea. (Kushoto) ni mwakilishi wa Nokia Magreth Tendwa.

Friday, December 14, 2012

RAIS KIKWETE KATIKA HAFLA YA MWAKA YA CONFEDERATION OF TANZANIA INDUSTRIES (CTI)


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijiandaa kumkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Distilleries Bw David Mgwassa (wapili kushoto), kombe la ushindi wa mwaka wa uzalishaji bora nchini katika hafla ya Shirikisho la Wenye Viwanda nchini  (CTI) usiku wa kuamkia leo Ijumaa Desemba 14, 2012 katika hoteli ya Serena Inn. Kulia ni Mwenykiti wa makampuni ya IPP Dkt. Rginald Mengi na Kushoto ni Bw. Arnold Kileo.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wafanyakazi na wadau wa  Tanzania Distilleries bada ya kunyakua   kombe la ushindi wa mwaka wa uzalishaji bora nchini katika hafla ya Shirikisho la Wenye Viwanda nchini  (CTI) usiku wa kuamkia leo Ijumaa Desemba 14, 2012 katika hoteli ya Serena Inn.PICHA NA IKULU
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa tayari kumkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Distilleries Bw David Mgwassa kombe la ushindi wa mwaka wa uzalishaji bora nchini katika hafla ya Shirikisho la Wenye Viwanda nchini  (CTI) usiku wa kuamkia leo Ijumaa Desemba 14, 2012 katika hoteli ya Serena Inn.Kushoto ni Bw. Arnold Kileo wa CIT
 Mzee Arnold Kileo akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Distilleries Bw David Mgwassa kwa kutwaa kombe la ushindi wa mwaka wa uzalishaji bora nchini katika hafla ya Shirikisho la Wenye Viwanda nchini  (CTI) usiku wa kuamkia leo Ijumaa Desemba 14, 2012 katika hoteli ya Serena Inn.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa nyanja mbalimbli za uzalishaji bora nchini katika hafla ya Shirikisho la Wenye Viwanda nchini  (CTI) usiku wa kuamkia leo Ijumaa Desemba 14, 2012 katika hoteli ya Serena Inn.

TBL YAKIPIGA JEKI KIKUNDI CHA MAMA WA KIMASAI

 Mkurugenzi wa Uhisiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo akimkabidhi mfanyakazi wa duka la Maasai Women Fair Trade Group cha Simanjiro, mkoani Arusha, Debora Mwingira mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 3.5 za kusaidia kulipia pango katika duka linalouza bidhaa zao Mtaa wa Kaunda Drive, Oyterbay, Dar es Salaam hivi karibuni.
Duka Maasai Trade Fair (kushoto) lililopo Barabara ya Kaunda Drive, Oysterbay,Dar es Salaam ambalo linauza bidhaa za asili zinazotengenezwa na kikundi cha kina mama wa Jamii ya Kimasai wa Simanjiro.

Monday, December 10, 2012

WIZARA YATENGA SH. BILIONI 8.9 KINUA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI NCHINI


 DODOMA, TANZANIA
Wizara ya Nishati na Madini imetenga jumla ya sh. bilioni 8.9 kwa dhamira ya kuwainua wachimbaji wadogo wa madini nchini ili kukuza kipato chao na hivyo kuboresha maisha yao. Aidha, jitihada za kuwainua wachimbaji wadogo zinalenga pia kuinua pato la taifa kutokana na kuongezeka kiwango cha kodi na tozo mbalimbali zinazopaswa kulipwa na wachimbaji hao kwa serikali.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alipokuwa akizungumza na wajumbe waliohudhuria mkutano mkuu wa mwaka wa wachimbaji wadogo wa madini nchini, uliofanyika mjini Dodoma tarehe sita na saba mwezi huu.

“Tunayo dhamira ya dhati kuwasaidia ili maisha yenu yaboreke na pia ili kukuza pato la taifa hili”, alisisitiza Waziri Muhongo na kuongeza kuwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ndilo limepewa jukumu la kusimamia mipango ya uendelezaji wachimbaji wadogo kwa kushirikiana na taasisi nyingine mbalimbali zinazohusika na sekta ya madini.

Hata hivyo Profesa Muhongo amewataka wachimbaji wadogo wa madini nchini kuhakikisha wanasajili biashara zao, kuanisha mapato yao, pamoja na kulipa kodi na tozo mbalimbali zinazowahusu ili taifa liweze kunufaika na rasilimali hiyo ya madini. Alisisitiza kuwa wachimbaji watakaofuata vigezo hivyo ndiyo tu watakaopata misaada ya aina mbalimbali ikiwemo mafunzo na mikopo kutoka serikalini na wadau wengine wa maendeleo.

Kwa upande wao, wajumbe waliohudhuria mkutano huo wa siku mbili, ambao ni viongozi na wawakilishi wa vyama vya wachimbaji madini kutoka mikoa yote nchini, waliahidi kuyafanyia kazi maagizo hayo ya Waziri kwa manufaa yao binafsi na ya taifa kwa ujumla.

Sunday, December 9, 2012

TRENI YA ABIRIA YAREJESHA SAFARI ZAKE MWANZA TANGU MWAKA 2009

Treni ikiwasili Jijini Mwanza leo

MWANZA, TANZANIA
MAMIA ya wakazi wa jiji la Mwanza, leo walilipuka kwa shangwe na vigelegele wakati wakiilaki Treni ya Abiria iliyowasili hapa kwa mara ya kwanza baada ya kusitishwa kwa safari zake toka Disemba 2009.

Treni hiyo iliwasili katika Stesheni ya mjini Mwanza saa 5:55 mchana, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba akiwa ni mmoja wa abiria waliopokewa na wananchi hao walioongozwa na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga.

Huku baadhi wakiwa na mabango yaliyobeba ujumbe mbalimbali wa kuipongeza Serikali na Waziri wa Uchukuzi Dk Halson Mwakyembe, wananchi hao walianza kushangilia mara tu Treni hiyo ilipotokeza kwenye yadi ya stesheni.

Shangwe hizo zilipokewa na abiria waliokuwemo ambao walionyesha nyuso za furaha na kuwapungia mikono wananchi na viongozi hao wakiwemo ndugu na jamaa waliokuwa wamefika kuwapokea.

“Hayawi hayawi leo yamekuwa, wao wao Treni ya abiria kuja Mwanza” ndivyo baadhi ya wananchi walivyosikika wakiimba wakati Dkt Tizeba akishuka pamoja na abiria wenzake na kupokewa na viongozi wa Chama na Serikali.

Pamoja na Konisaga aliyekuwa akimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, wengine waliipokea Treni hiyo ni pamoja na Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Amina Masenza, Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula na katibu wa CCM wilayani Nyamagana, Deogratias Rutta.

Baadhi ya abiria wakiwemo Mwaka Hussin mkazi wa Tabora na Moshi Mfalila mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es salaam , wakizungumza na Uhuru walisema kuwa wanaishukuru serikali kurejesha ufasiri huo wa wanyonge.

“Tunaishukuru serikali usafiri huu mzuri, japo viti vya mabehewa naona vimechoka, waviboresha na kudhibiti vibaka wasiingie ovyo.” Alisema Hussein huku Mfalila akidai kuwa waboreshe Injini za usafiri huo ili abiria wasikwame tene kama walivyokwama juzi kwa saa nne, Ubungo.

Wakazi wa jiji la Mwanza waliofika kuilaki Treni hiyo, wakiwemo Sikitu Chibulule, Nelson Wilson na Mwanaidi Rajabu, walimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kutekeleza ahadi aliyoitoa ya kufufu usafiri wa Reli na kusema kuwa serikali ya CCM sasa inafurahisha kwa uchapa kazi.

Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa TRL nchini, Kipallo Kisamfu alisema kuwa, shirika lake lina furaha isiyo kifani kuwasili kwa Treni hiyo Mwanza, siku ambayo ina historia ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara.

“Disemba 2009 niyo ilikuwa mara ya mwisho Treni hii kuja Mwanza safari zake zikasitishwa, lengo letu ni kurudisha ufanisi wa Treni uliokuwepo awali, lengo hilo si jepesi ni zito lakini kwa hali tuliyofikia tutafika huu ni mwanzo tu wa jitihada za serikali yetu.” Alisema Kisamfu.

Alieleza kuwa mpango wa serikali ni kuhakikisha Treni inafufuka na kutoa mchango wake mkubwa katika huduma za jamii na kukuza pato la taifa, hivyo pamoja na kuanza na mabehewa machache, huduma hiyo itaboreka siku hadi siku kwani ukarabati wa mabehewa mengine na vichwa vya Treni, unendelea.

Saturday, December 8, 2012

MKURUGENZI MKUU WA EABC AKUTANA NA WANAHABARI WA EAC KATIKA MAFUNZO

Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Jumuia ya Afrika Mashariki, Andrew Luzze Kaggwa, akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari juu ya Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kuangalia Utekelezaji wa Masuala ya Soko la Pamoja. Mafunzo hayo yanahusisha wanaandishi wa habari kutoka nchi zote wanachama wa EAC, na kufanyika Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Jumuia ya Afrika Mashariki, Andrew Luzze Kaggwa, akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari juu ya Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kuangalia Utekelezaji wa Masuala ya Soko la Pamoja. Wengine pichani ni washiriki wa mafunzo hayo.
Katibu wa baraza la Asasi za Kijamii la Jumuia ya Afrika Mashariki, Dk. Martin Mwodha, akizungumza katika mafunzo hayo juu ya ushiri wa Asasi za kiraia katika ulelimishaji na ufikishaji wa elimu ya Soko la Pamoja la EAC.
Mchambuzi wa Siasa za Afrika ambaye pia ni Mwanahabari Mkongwe nchini Tanzania, Jenerali Ulimwengu akitoa mada katika mafunzo hayo leo.
Dawati la ufundi nalo wakati wote lilikuwa katika wakati mgumu wakuhakikisha kila kitu kinaenda sawa. Kutoka kushotoni Aline Ellermann, Elizabeth Wanyoike na Hussein Karim wote kutoka ofisi ya GIZ ambao ndio wawezeshaji mafunzo hayo yaliyoandaliwa pamoja na AC
Kuna wakati mambo yanaonekana hayaendi na hapa anaonekana Elizabeth Wanyoike (kulia) akikuna kichwa) huku Aline Ellermann akiendelea na kazi.
Fiona Mbabazi kutoka Rwanda akimshukuru Ofisa mtendaji wa EABC, Andrew Kaggwa kwa maelezo juu ya Baraza hilo.Kati ni Jenerali Ulimwengu na Aline Ellermann.
Bizimana Jean-Marie akitoa zawadi kwa Dk. Martin Mwadha wa Asasi za Kiraia za EAC, wengine pichani kutoka kushoto ni Elizabeth Wanyoike wa GIZ, Balozi  Jeremy Ndayiziga, Andrew Kaagwa na Jenerali Ulimwengu.:Picha zote na Mroki Mroki wa Father Kidevu Blog

TANGAZO LA M-PESA YATENGAMAA TENA


Huduma ya M-Pesa ilipata hitilafu jana.
  Kufuatia hitilafu hiyo wahandisi wa mtandao Tanzania wakishirikiaana na wadau wa nchini Uingereza walifanya kazi usiku na mchana ili kutatua tatizo na hatimaye kuwezesha huduma kufanya kazi mida ya jioni.
  Mkurugenzi  wa kitengo cha M-Pesa, Jacques Voogt  amesema  wateja walikua wakipiga  *150*00#   wanapata ujumbe mfupi SMS usemao “Ndugu mteja, huduma ya M-Pesa haipatikani kwa sasa, tafadhali jaribu tena”
  Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kwa wateja wetu, mawakala wa M-pesa na wadau wetu wote kwa ujumla.
M-Pesa ni huduma pendelevu ya malipo kwa wateja zaidi ya milioni 4.5 na ina wadau wa biashara zaidi ya 200 wanaotumia huduma hii kukusanya na kusambaza pesa.

Friday, December 7, 2012

KITWANGA AHITIMISHA ZIARA KATIKA VIWANDA NA MAHOTELI JIJINI NA KUKEMEA WANAOCHAFUA FUKWE ZA BAHARI


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga (wa tatu kulia) akiwasili katika Kiwanda cha kutengeneza dawa za binadamu cha Shelys kilichopo Mwenge jijini Dar huku akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo ( wa pili kulia), Mkurugenzi wa Kurugenzi ya kufanikisha udhibiti wa Mazingira Mhandisi Dr. Robert Ntakamulenga na Wataalamu wa Kitengo cha Mazingira kutoka katika Wizara yake katika muendeleo wa ziara za kushtukiza Viwandani kukagua mfumo wa mazingira ya maji taka yenye kemikali katika viwanda hivyo kama unaendana na viwango vilivyowekwa.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akieleza dhumuni la ziara yake katika kiwanda hicho kwa Afisa Rasilimali watu wa Kiwanda cha dawa cha Shelys Bw. Nissa Mwaipiana (kulia).
Mkuu wa Idara ya Kuhakiki ubora wa Kiwanda hapo Bi. Shemina Pera Somji akitoa maelezo kwa Naibu Waziri na Ujumbe wake.
Mkuu wa Idara ya Kuhakiki ubora wa Kiwanda hapo Bi. Shemina Pera Somji akimwongoza Mh. Charles Kitwanga kwenda kukagua sehemu ya kutibu maji taka yenye kemikali.
Mwendesha Mashine wa Kiwanda hicho Bw. Patrick Mapunda (mwenye koti) akitoa ufafanuzi Kwa Naibu Waziri Mh. Charles Kitwanga wa namna wanavyokusanya na kuyatibu maji taka yanayotokana na uzalishaji kiwanda hapo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akitoa maagizo wa NEMC baada ya kutoridhishwa na mfumo wa maji taka ya kiwanda hicho kutofikia ubora unaotakiwa.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga(wa pili kulia) akiongozwa na Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha soda cha CocaCola cha jijini Dar Bw. Ernie Van Vreden (kulia) kwenda kukagua maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho. Country PAC Manager wa kiwanda hicho Bw. Evans Mlewa (wa pili kushoto) na kurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo.
Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha soda cha CocaCola cha jijini Dar Bw. Ernie Van Vreden akitoa Maelezo kwa Mh. Kitwanga juu ya Mitambo Mipya ya Kisasa yenye kiwango cha Kimataifa kwa ajili ya kutibu maji taka katika Kiwanda hicho.
Mh. Kitwanga na Ujumbe wake ukitizama Bwawa la Samaki linalotumika kufanyia majaribio ya maji taka ambayo yamekwisha safishwa kwa ajili ya matumizi mengine kiwandani hapo.
Mh. Charles Kitwanga (kulia) akitoa maoni yake baada ya ziara ya kukagua maeneo mbalimbali ya kiwanda cha CocaCola na kuridhishwa na utaratibu unaotumika katika uzalishaji wa bidhaa zao na mfumo wa kuhifashi maji taka na kuyasafisha kwa njia ya kisasa na kuitaka kampuni hiyo iwe mfano wa kuigwa na iwe Mwalimu kwa Makampuni mengine.
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Soda cha CocaCola Bw. Basil Gadzios (katikati) akitoa shukrani kwa Mh. Naibu Waziri na kuahidi kutoa ushirikiano wa kitaalam kwa viwanda vingine juu ya utunzaji wa maji taka na namna ya kuyasafisha kisasa kuepuka kuharibu Mazingira na kuongeza kuwa Kampuni ina mkakati kabambe kwa mwaka 2013 kutengeneza ajira kwa vijana ambapo inakusudia kujenga vituo katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya vijana kukusanya chupa za plastiki zinazotokana na kiwanda hicho kwa ajili kuzalishwa upya.
Naibu Waziri Mh. Charles Kitwanga katika picha ya pamoja na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha CocaCola Bw. Basil Gadzios na Ujumbe wa NEMC na Maafisa wa Wizara yake.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga (wa pili kushoto) akiwasili katika Hotel ya White Sands jijini Dar es Salaam kujionea jinsi Hoteli hiyo iliyopo ufukweni mwa bahari inavyotunza mazingira yake. Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya White Sands Alwyn Kellerman na Afisa Mazingira wa Hoteli hiyo Bi. Linda Mbuya.
Mmoja wa wafanyakazi wa Hoteli hiyo akifunua chemba inayopitisha maji taka kwa ajili ya kukaguliwa na jopo la wataalam kutoka NEMC na Maafisa wa Wizara. Katika ukaguzi huo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga hakuridhishwa na jinsi hoteli hiyo inavyoendesha mfumo wake wa maji taka na kuagiza timu ya wataalam kutoka NEMC kufanya ukaguzi upya wa mifumo hiyo.
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Giraffe Ocean View Bw. Nicholas Oyieko akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Mh. Kitwanga (wa pili kushoto) jinsi hoteli hiyo inavyotunza mazingira na namna inavyodhibit mfumo wake wa maji taka kuhakikisha kwamba haileti madhara.
Hii ni sehemu iliyoko pembeni ya Hoteli ya Giraffe ambayo mmiliki wake hafahamiki ambayo imewekwa uzio na kufanya bahari kushindwa kupumua vizuri na kusababisha mkusanyiko wa uchafu unaodaiwa kutuama mahali hapo tangu mafuriko ya hivi karibuni yaliyoikumba jiji la Dar es Salaam. Naibu Waziri ameamuru muhusika kutafutwa mara moja na kupigwa faini na kuamuriwa kuondoa vifusi hivyo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga na ujumbe wake wakiangalia eneo hilo.
Mh. Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Bw. Sven Lippinghof baada ya kuwasili hoteli hapo kwa ziara ya kushtukiza kukagua miundo mbinu ya maji taka kwa hoteli zilizopo pembezoni mwa fukwe za bahari ya Hindi.
Mh. Charles Kitwanga akielekea kufanya ukaguzi wakati wa ziara yake ya kutembelea hoteli mbalimbali za jijini Dar es Salaam zilizopo pembezoni mwa fukwe za bahari ya Hindi.
Wataalamu kutoka NEMC na Maafisa wa Wizara wakikagua moja ya chemba za hoteli hiyo zilizounganishwa na mabomba yanayochuruzisha maji baharini ambapo Hoteli hiyo ilidanganya kwa kusema kwamba kila chemba hizo zinapojaa wanaita gari maalum la kunyonyea maji taka hayo kitu ambacho si kweli kwa mujibu wa watalaam wa NEMC.
Moja ya bomba la maji taka kutoka katika hoteli hiyo yanayotiririkia baharini.
Pichani ni Matundu ya mabomba ya maji machafu yanayotokea Hoteli ya Double Tree By Hilton yaliyoelekezwa baharini.
Naibu Waziri Mh. Charles Kitwanga akitoa amri kwa Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo ambapo ametoa muda wa miezi miwili kwa uongozi wa Hoteli ya Double Tree kutafuta njia nyingine ya kumwaga maji taka isiyochafua fukwe na maji ya bahari akisema kuwa yeye si mzungumzaji sana bali anasimamia vitendo. Mheshimiwa Waziri amemtaka Bwana Mchallo kusimamia utekelezaji wa zoezi hilo.
Mwanasheria wa NEMC Bw. Mwanchane Heche akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema watachukua hatua kuanzia kesho (7 Disemba 2012) kwa kuwa Afya za watu hazisubiri muda hivyo tunauwezo wa kumfungia biashara yake, kumlipisha faini au vyote kwa pamoja na tutahakikisha anaacha kumwaga maji taka eneo la baharini.
Mwanasheria wa NEMC Bw. Mwanchane Heche akimpa utaratibu wa mamlaka yake hatua itakayochukua Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Bw. Sven Lippinghof akimweleza kuwa japokuwa huduma zao ni bora mfumo wao wa maji taka unahatarisha Afya za Wananchi na kuharibu Mazingira.
Huu ni muonekano wa Hotel ya Double Tree By Hilton kwa nyuma Upande wa bahari ambako ndiko wateja wao wanakopumzika na kupunga upepo mwanana wa baharini kunakomwagwa maji machafu ya kinyesi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga ( wa pili kushoto) akizungumza na Meneja Mkuu wa Hoteli ya Coral Beach Hans Heuer (kushoto) ambako alihitimisha ziara yake.
Mh. Charles Kitwanga na Ujumbe wake wakikagua miundo mbinu ya eneo la Coral Beach Hoteli.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akitoa maoni yake kwa Uongozi wa NEMC na kusema kuwa ameridhishwa na hali ya mazingira na utaratibu unaotumiwa na Hoteli hiyo.

Tuesday, December 4, 2012

AIRTEL YAZINDUA PROMOSHENI YA MWISHO WA MWAKA 2012 KWA WATEJA WAKE

* Ni promosheni  ya "AMKA MILIONEA".
* Ndani ya siku 90 wateja 875 wa Airtel kuzoa sh. milion 401


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua promosheni mpya ili kuweza kuwazawadia wateja wake wakati wa msimu huu wa mwisho wa mwaka.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo kwa waandishi wa habari  Meneja wa huduma za ziada wa Airtel Francis Ndikumwami alisema kwamba "Airtel  inakutoa fursa nyingine kwa Tanzania kushiriki na kushinda zawadi ya fedha taslimu wakati wa msimu huu wa sherehe. Leo tunazinduzi "AMKA MILIONEA" amabazo jumla ya zawadi za fedha taslimu zenye thamani ya shilingi milioni 401zitatolewa ndani ya siku 90 tu.

Kutakuwa na washindi wa kila siku, kila wiki, kila mwezi na zawadi kubwa moja itatolewa mwisho wa promosheni, katika promosheni hii wateja wa Airtel 875 watazawadia hizo milioni 401.

AMKA MILIONEA itakuwa na washindi wa aina tofauti tofauti . Washindi wa kila siku, kila wiki na kila mwezi, AMKA MILIONEA itahakikisha kila siku kunawashindi 10 kushinda kila siku na watagawana jumla ya shilingi  3,000.000, kila wiki jumla ya shilingi milioni 6,000,000 zitashindaniwa na washindi 10 na kila  mwisho wa mwezi  mshindi mmoja atashinda kitita cha shilingi milioni 30 wakati milioni  50, 0000 Tshs itaenda kwa mshindi mmoja mwisho wa promosheni hii.

Akizungumza jinsi ya kujiunga na promosheni hiyo  Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema, Ili mteja aweze kushiriki inabidi atume neno WIN/SHINDA kwenda namba 15595 bure na utakuwa ujiungajiunga, Baada kujiunga mteja atakuwa atapata ujumbe kutoka 15656 na kupata maswali ambayo atajibu na akipata sahihi atapata ponti 20 akikosea atapata ponti 10. Na kwakila ujumbe atakaotuma atatozwa kiasi cha shilingi 350 pamoja na kodi.

Amka milionea imeanza leo Desemba 3, 2012 itaenda hadi Machi 2, 2013

Vigezo Muhimu
Mshiriki mmoja hawezi kushinda zaidi ya 1 ya kwa zawad ya kila siku .
Mshiriki mmoja hawezi kushinda zaidi ya 1 yakwa zawadi ya kila wiki
Mshiriki mmoja hawezi kushinda zaidi ya 1 zawadi ya kila mwezi.
Mshiriki mmoja unaweza kushinda mara moja zawadi ya kila siku, mara
moja zawadi ya kila wiki  na mara 1 zawadi ya kila mwezi. Lakini pia
anaweza akajishindia zawadi kubwa ya mwisho wa promosheni

Kujiunga
Tuma neno "WIN / Shinda", kwenda namba 15595 ( bure), na kisha utapokea ujumbe wa ukaribisho utakaombatana na maswali utakayojibu.

Kila jibu sahihi mteja atapata pointi/alama 20 na akikosea atapata pointi 10 zitakazomuwezesha kushinda, ukijibu maswali mengi unajiongezea nafasi ya ushindi